Morsi akabidhiwa madaraka na Tantawi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 30 June 2012

Morsi akabidhiwa madaraka na Tantawi

Rais Mohamed Morsi wa Misri


Rais wa kwanza wa kiraia wa Misri, na kutoka chama cha Kiislamu, Mohammed Morsi, ameapishwa, na ametoa wito kuwa bunge la nchi lirejeshwe haraka - bunge lilofutwa hivi karibuni.
Hapo awali, akitoa hotuba yake ya kwanza iliyogusia mambo mengi, katika Chuo Kikuu cha Cairo, Bwana Morsi alisema atalilinda jeshi kama taasisi, lakini piya alionya jeshi halifai kuwa mbadala wa matakwa ya wananchi.Katika sherehe kwenye eneo la jeshi nje ya Cairo, kiongozi wa wakuu wa jeshi wanaoongoza nchi, Field Marshal Mohammed Tantawi, alikabidhi madaraka rasmi kwa Rais Morsi.
Bwana Morsi aliahidi ukurasa mpya utaong'ara katika historia ya nchi, kufwatilia ule aliosema ni ukurasa wa kuchusha.
Alipokuwa akizungumza, akina mama ambao watoto wao waliuliwa chini ya utawala wa Rais Mubarak, walibeba juu picha za watoto wao hao wa kiume.
Bwana Morsi piya alisema Misri haitotapakaza mapinduzi nchi za nje.
Rais mpya aliapishwa kwenye sherehe iliyofanywa katika mahakama ya katiba mjini Cairo.

No comments:

Post a Comment