Jengo pekee lililosalia baada ya bomu la Atomic kutoa na kusambaratisha mji wa Hiroshima. Hivi sasa jengo hilo limehifadhiwa kati hali yake kwa kumbukumbu ya tukio hilo
Mzee. Keijiro Matsushima akisumulia hadidhi yake kwa waheshimiwa Wabunge jinis alivyonusurika siku bomu hilo lilipo lipua mji huo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini mmoja wa mashuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee. Keijiro Matsushima siku lilipoteketeza mji wa Hiroshima tarehe 6 Agosti 1945 ambapo zaidi ya watu 66,000 walifariki 92,000 hawakujulikana walipokuwa mpaka sasa na 129,558 walijeruhiwa vibaya. Mzee Matsushima alikuwa na umri wa miaka 16 siku hiyo na siku ya mlipuko alikuwa darasani km 2 katika chuo cha Hiroshima Technical College ambapo katika darasa alilokuwapo wanafunzi kadhaa walifariki pia kutokana na mionzi mikali ya bomu hilo. Hivi sasa Mzee Matsushima ana miaka 83. Kushoto kwa Mhe. Spika ni Mhe. Godfrey zambi na Mhe. Anne Kilango Malecela
Mzee. Keijiro Matsushima akielezea kwa hisia jinsi alivyojikongoja kuukimbia mji wa Hiroshima huku akipisha na mamia ya wakazi wa eneo hilo wakio wanakimbia na huku ngozi zao zikinyofoka
Shuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee. Keijiro Matsushima akiwaonesha katika ramani waheshimiwa Wabunge na Mhe. Spika eneo alipokuwa siku bomu linalipuka na sehemu bomu lilopolipukia.
Mzee. Keijiro Matsushima akielezea jinsi alivyoona mwanga Mkali wakati Bomu hilo likishuka
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika Picha ya Pamoja na Mzee. Keijiro Matsushima shuhuda aliyenusurika katika Bomu la Atomic lilisambaratisha mji wa Hiroshima
Mhe. Tundu Lissu akiuliza swali kuhusu mda uliochukua kuujenga upya mji huo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakioneshwa na Ndg. Koichiro Maeda Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima mchoro wa madhara ya Bomu la Atomic lilirushwa katika Mji wa Hiroshima wakati wa vita kuu ya pili mwaka 1954 jinsi mji huo ulivyokuwa siku hiyo baada ya kulipuliwa.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakitizama picha iliyopigwa baada ya kulipuliwa Mji wa Hiroshima mwaka 1945 na Bomu la Atomic. Picha hiyo ilipigwa tarehe 6 agosti 1945 mda mchache baada ya kulipuliwa kwa mji huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi Ndg. Koichiro Maeda Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima ujumbe kutoka kwa timu ya wabunge aliongozana nayo ziara hiyo wenye kulaan matumizi ya silaha za Nuclear Dunian.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha Kumbukumbu na kuandika ujumbe wa kulaani matumizi ya silaha za Nuclear baada ya kumaliza kutembelea makumbusho yenye picha na matukio yaliyotokea siku bomu la Atomic lilivyo sambaratisha mji wa Hiroshima.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
No comments:
Post a Comment