MHE.BALOZI JUMA MWAPACHU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA DODOMA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday, 3 October 2011

MHE.BALOZI JUMA MWAPACHU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA DODOMA



















Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa  Jamhuri  ya  Muungano   wa Tanzania amemteua Balozi  Juma   Mwapachu  kuwa    Mwenyekiti   wa    Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma kuanziatarehe 14 Septemba 2011.Atakuwa kwenye  nafasi  hiyo kwa kipindi cha miaka  minne (4)
Balozi Mwapachu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kwanza na sasani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na njeya nchi zikiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya AfrikaMashariki, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ikijumuisha  nchi za Uhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria. Aidha Mhe. Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini naamewahi kushika nyadhifa za juu katika Taasisi za Umma na binafsi.Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wabaraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mhe.Balozi Juma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki naalikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunga na Jeshi la Polisi nchini.
Mhe.Balozi Juma Mwapachu aliwahi kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wafalsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam naamewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.
Uongozi wa Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu cha Dodoma inamkaribisha na kumtakia kila la kheri .....
Balozi Juma Mwapachu katika majukumu yake mapya.

na Fullshangwe blog

No comments:

Post a Comment