TIGO WADHAMINI WAKUU WA BONGO STAR SEARCH ACADEMY 2011 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Aug 2011

TIGO WADHAMINI WAKUU WA BONGO STAR SEARCH ACADEMY 2011


BSS Second Chance 2011 ni kipindi kinachoongoza kwa kuwa na watazamaji wengi na kinachopendwa sana Tanzania, kipindi hiki kinachoprekodiwa Mbalamwezi Beach Club na kurushwa hewani na ITV siku ya Ijumaa saa 12:15 jioni,jumamosi saa 3:00 usiku na kurudiwa siku ya jumanne saa5:00 usiku.
Dhumuni kubwa leo ni kuwatambulisha kwenu wadhamini wapya ambao wanatambua na kuthamini vipaji vya Tanzania na wamekuwa nasi bega kwa bega ili kuhakikisha BSS second chance inachukua sura na mwonekano mpya kwa watazamaji.
Wadhamini hao ni TIGO,PSI(Salama Condoms),CHAMPION(Egender Health),NSSF na GOLDEN TULIP HOTEL.Tunawashukuru sana kwa mchango wao mkubwana tunawakaribisha waendelee kuwa nasi katika BSS zinazofuatia.
Kama kawaida kila mwaka Benchmark imeongeza dau la zawadi ili kuboresha na kubadilisha maisha ya washiriki, Mwaka huu jumla ya shil
ingi milioni 55 zitashindaniwa na washiriki wa shindano hilo.
Napenda kuwatambulisha kwenu washiriki waliofanikiwa kuingia kumi bora ambao ni;Rogers Lucas BSS no.(23),Bella Kombo BSS no.(5),Chibi Dayo BSS no.(7),Sarafina Mshindo BSSno.(24),Hajji Ramadfhani BSS no.(11),Mary Banyukwa BSS no.(15),Mary Lucos BSS no.(16),Waziri Salum BSS no.(27),Beatrice WilliamBSS no.(4) na Imani Lissu BSS(I2).Ingawa tayari wamebaki washiriki tisa baada ya mary Banyukwa BSS no.(4) kuondolewa katika mashindano haya wiki iliyopita.
Pia sina budi kuwashukuru TBL kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro premium lager kwa udhamini wao wa miaka mitatu,Paradise express hotel,shoprite supermarket,shear illusion,Fly540,Photo point,Biggy respect,Kilimanjaro drinking water,AAR health care,SELCOM na emirates barbershop ambao tuko nao kwa muda mrefu.
Nawashukuru sana.Vilevile natoa shukrani zangu za dhati kwa Turn Around Academy ambao ndio wanawafundisha washiriki katika BSS Second Chance 2011 Academy ambayo iko katika hoteli ya kifahari ya Golden tulip.
Benchmark inawashukuru wote kwa kufika na endeleeni kuwapigia kura washiriki mnaowapenda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad