RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AMEREJEA NCHINI BAADA YA ZIARA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA KUTOKA CANADA NA MAREKANI. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

1 Oct 2013

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AMEREJEA NCHINI BAADA YA ZIARA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA KUTOKA CANADA NA MAREKANI.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Wanaofuatia ni Mbunge wa Nkenge Mhe. Asumpta Mshama na Mbunge wa Wawi Mhe Hamad Rashid Mohamed.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakilakiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Rita Mlaki alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Picha na IKULU ---- THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nchini mchana wa  jana Jumatatu, Septemba , 2013, baada ya ziara ya kikazi yenye mafanikio makubwa katika Marekani na Canada.

Miongoni mwa shughuli nyingine nyingi katika ziara hiyo, Rais Kikwete alihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini Jumapili ya Septemba 15 alianzia safari yake mjini San Francisco, Marekani, ambako miongoni mwa mambo mengine alizindua Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika Jimbo la California. 

Rais pia alikutana na kuzungumza na Jumuia ya Watanzania katika Jimbo hilo na kukaribishwa katika Jiji la Vallejo katika sherehe za miaka 20 za uhusiano wa kimji kati ya Jiji hilo na mji wa Bagamoyo.

Ziara ya Rais Kikwete San Francisco ilifuatiwa na ziara ya mjini Washington ambako shughuli zake kubwa zilikuwa kukutana na viongozi wa Bunge la Marekani na pia kuhudhuria Hafla ya Chakula cha Usiku cha Taasisi ya Kulinda Hifadhi na Mazingira ya Bunge la Marekani (ICCF) ambako alitunukiwa tuzo maalum za Mtunzaji Mazingira Bora wa Mwaka. 

Aidha, Rais Kikwete alishuhudia utiaji wa saini mikataba ya kufungua Ofisi Ndogo za Ubalozi wa Tanzania katika majimbo mbali mbali ya Marekani.

Baada ya hapo, Rais Kikwete alikwenda Canada ambako alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Sheria na Chuo maarufu na kikongwe cha Canada cha Guelph ambacho ni maarufu duniani kwa shughuli na utafiti wa kilimo.

Kufuatia ziara hiyo ya Canada, Rais Kikwete alikwenda New York ambako alikuwa na shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN Ijumaa ya wiki iliyopita, akakutana na Katibu Mkuu wa UN Mheshimiwa Ban Ki Moon, akashiriki kikao maalum cha wakuu wa nchi kujadili hali ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kilichoitishwa na Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Akiwa mjini New York, Rais Kikwete pia alikuwa kiongozi pekee wa Afrika aliyealikwa kushiriki katika Mkutano wa Rais wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama na taasisi zisizokuwa za kiserikali duniani na pia alihudhuria Halfa Maalum iliyoandaliwa na Rais Obama alipomaliza kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN.

Aidha, Rais Kikwete alishiriki Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Clinton Global Initiative na pia akawa mzungumzaji rasmi katika Mkutano wa Kupambana na Ujangili Duniani uliotishwa na Rais Ali Omar Bongo Ondemba wa Gabon.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
30 September 2013

No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633