Wadau wa Michezo nchini wakizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha;kutoka kushoto ni Gadiel Urio PR wa Shughuli hiyo, Rogath John Stephen(Mwanariadha wa kimataifa na Mtoto wa John Stephen Akhwari) , Bw. Wilhelm Gidabuday ambae ni mwanariadha na mwanaharakati wa Michezo Tanzania na Phaustin Baha Sule Mwana Riadha na Mshindi wa medali ya nusu marathon. |
Hapa wakipewa maelekezo na PR wa shughuli hiyo,kabla ya kuanza kwa mazungumzo na Vyombo vya Habari ,katika mkutano wa vyombo vya habari vilivyofanyika Jijini Arusha. | . |
**********************
Maandishi na Gadiel Urio -Arusha
“Sisi
kama wadau wakubwa na wazalendo wa
michezo Tanzania ,tumeamua kuanzisha tukio hili la harambee, kupitia kukimbia mbio za
kupokezana vijiti (RELAY MARATHON) , ili kuchangisha pesa ya kuanzisha kiijiji cha kitaifa cha Michezo nchini
Tanzania .pia kijiji hicho cha michezo
Tanzania kitaitwa “John Stephen Akhwari National
Sports Village” ,kwa heshima ya mwanariadha huyo wa kimataifa alieiletea sifa
nchi ya Tanzania kwa kukimbia bila kukata tamaa ,hata aliposhindwa alidiriki
kusema “Nchi yangu haijanituma kuja kuanza mashindano: bali kumaliza
Mashinadano. Pia baada ya kuona michezo mingi
Tanzania imekosa vituo vyenye hadhi ya kimataifa vya kufanyia mazoezi yenye
ubora wa kimataifa,ili kupata medali ndani na nje nchi yetu. Hivyo tukakaa na baadhi ya wanariadha wazalendo
nchini kama vile,Phaustin Baha na Rogart John Stephen ,ili tufanye tukio hili la
kihistoria ambalo hakuna mwingine aliewahi kujaribu kulifanya “alisema Wilhem
Gidabuday
“Mashindano
hayo yatakuwa ya mbio za kupokezana
vijiti yaani (RELAY MARATHON) kuanzia Magogoni jijini Dar es Salaam (IKULU) na
kumalizia jijini Arusha (Sheikh Amri
Abeid) kupitia barabara kuu itokayo Dar es Salam hadi Arusha, yenye takribani
kilomita zisizopungua mia saba (700 Km). Mbio hizo zitahusisha wanariadha wa tano maarufu na wazalendo na ambao wamewahi kukimbia na
kuiletea nchi yetu sifa kimataifa”.aliongeza Bw. Gidabuday
Malengo
ya Mbio hizi ni:
Moja ; kuwezesha kuanzisha kijiji
cha michezo Tanzania kulingana na jeografia ya nchi yetu ilivyo, kuwa na maeneo
ya nyanda za juu kaskazini na kusini ambamo hali ya hewa inaruhusu michezo
mingi kufanyika ikiwemo mchezo wa riadha. hili litasaidia kupata wanamichezo
wazuri na wenye lengo la kuiletea sifa na medali nchi yetu kitaifa na kimataifa
na kuongeza ajira kwa wanamichezo wetu.
Pili ;kwa kuwa Raisi wetu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya
Kikwete ni msikivu ,anapenda michezo na alitambua mchango mkubwa wa mwanariadha
mkongwe Bw. John Stephen Akhwari na kumpa Tuzo ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania
,ndipo tukapendekeza kijiji hiki cha michezo kiitwe John Stephen Akhwari, ila kijiji
hiki ni mali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mashindano haya yanatarajiwa
kufanyika kabla ya mwezi wa sita mara tu
tutakapowapat a wahisani,Serikali na wadau wengine wa michezo kujitokeza
na kuwezesha jambo hili kutimia . hivyo
tunaiomba serikali ,wadau mbalimbali wa michezo nchini pamoja na wahisani
wajitokeze ili kutimiza lengo hili la kitaifa la kuanzisha kijini cha michezo cha
John Stephen Akhwari.
Mwisho
;Mwaka ujao wa 2014 tunatarajia kukimbia mbio zingine kutoka Bagamoyo hadi
ujiji ,katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar ,lengo ni kuhamasisha na kuchangisha
pesa za ujenzi wa kituo hicho cha kimataifa.
No comments:
Post a Comment