Spika wa
Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwasili katika jengo
jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha kwa lengo la kuzindua Ukumbi
wa Bunge la Afrika Mashariki ulioko katika jengo hilo.
Spika wa
Bunge la Africa Mashariki Mhe. Margret Natongo Zziwa (kulia) akimkaribisha Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda katika jengo hilo.
Spika wa
Bunge Afrika Mashariki,Mhe. Margret Natongo Zziwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) ili kulihutubia
Bunge la Afrika Mashariki.Kulia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne
Makinda.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la
Afrika Mashariki wakati alipofika kuzindua Ukumbi Mpya wa Bunge la
Afrika Mashariki ulioko katika jengo jipya la Jumuiya ya Afrika
Mashariki Jijini Arusha.
Baadhi ya
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais
Jakaya Kikwete.
Jengo jipya
la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Prosper Minja- Bunge.
No comments:
Post a Comment