Utalii : Tanzania Kuingia kwenye Ramani ya Kimataifa ya Utalii wa Mikutano (MICE) - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Thursday, 7 August 2025

Utalii : Tanzania Kuingia kwenye Ramani ya Kimataifa ya Utalii wa Mikutano (MICE)

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Popular Links, Bi. Mariam Ndabagenga, alisema Tanzania ina kila rasilimali muhimu kuiwezesha kuwa kitovu cha utalii wa mikutano Afrika.

“Tuna miundombinu ya kisasa, hoteli bora, vivutio vya asili na wataalamu wa kuandaa matukio makubwa. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kuwa na chombo maalum cha kusimamia sekta hii,” alieleza Bi. Ndabagenga.

Aliongeza kuwa ni muhimu wageni wanaokuja kwa ajili ya mikutano wapewe huduma bora na pia waelekezwe kutembelea vivutio vya utalii nchini ili kuongeza mapato kwa sekta nyingine.

Dar es Salaam - Serikali ya Tanzania imechukua hatua madhubuti katika kuimarisha sekta ya Utalii wa Mikutano, Maonesho, Makongamano na Safari za Motisha (MICE), ikiwa ni mkakati wa kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumza katika Jukwaa la Wadau wa Sekta ya MICE lililofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Ernest Mwamaja, alieleza kuwa serikali imeazimia kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha mikutano barani Afrika.
"Serikali imeshaweka wazi kuwa utalii wa mikutano ni zao la kibiashara lenye uwezo mkubwa wa kuongeza mapato ya taifa na kuchochea shughuli za kiuchumi," alisema Bw. Mwamaja.

Katika jukwaa hilo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliwasilisha tathmini ya mwenendo wa sekta ya MICE, ikieleza fursa zilizopo pamoja na changamoto zinazokabili sekta hiyo. Miongoni mwa maendeleo makubwa yaliyotajwa ni ujenzi wa ukumbi mpya wa mikutano jijini Arusha wenye uwezo wa kuchukua watu 5,000, hatua inayolenga kuvutia mikutano ya kimataifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Popular Links, Bi. Mariam Ndabagenga, alisema Tanzania ina kila rasilimali muhimu kuiwezesha kuwa kitovu cha utalii wa mikutano Afrika.

“Tuna miundombinu ya kisasa, hoteli bora, vivutio vya asili na wataalamu wa kuandaa matukio makubwa. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kuwa na chombo maalum cha kusimamia sekta hii,” alieleza Bi. Ndabagenga.

Aliongeza kuwa ni muhimu wageni wanaokuja kwa ajili ya mikutano wapewe huduma bora na pia waelekezwe kutembelea vivutio vya utalii nchini ili kuongeza mapato kwa sekta nyingine.
“Tofauti na aina nyingine za utalii, MICE haina misimu maalum. Hii ni fursa ya kuongeza mapato ya nchi kwa kipindi chote cha mwaka,” alisema.

Katika jukwaa hilo, washiriki walipata mafunzo kuhusu sheria, taratibu za manunuzi na mikataba, kupitia warsha iliyoendeshwa na Bw. Paul Bilabaye kutoka taasisi ya Uongozi. Alisisitiza umuhimu wa utoaji wa huduma bora na kuzingatia masharti ya mikataba.

“Ukipata zabuni leo ukaharibu, unaharibu sifa ya nchi, si kampuni yako pekee,” alionya Bw. Bilabaye.
Jopo la majadiliano pia lilihusisha wataalamu kutoka TTB, BASATA, TRA na BRELA kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya usajili wa biashara na uwekezaji kwenye sekta ya MICE.

Jukwaa hilo lilihitimishwa kwa tafrija mchapalo (networking cocktail), ambapo wadau walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.

Tukio hilo limeandaliwa na kampuni ya Popular Links kwa kushirikiana na BASATA, na limepongezwa na wadau kama hatua muhimu ya kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya utalii wa mikutano.

No comments:

Post a Comment