Kimataifa : JK Ashiriki kutoa mafunzo chuo kikuu cha Havard huko Boston kwa mawaziri wa nchi zinazoendelea - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 29 April 2025

demo-image

Kimataifa : JK Ashiriki kutoa mafunzo chuo kikuu cha Havard huko Boston kwa mawaziri wa nchi zinazoendelea

IMG-20250428-WA0232-860x573


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yuko mjini Boston, Marekani, ambako anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea.

Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard, maarufu kama Harvard Ministerial Leadership Program, unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu walioalikwa kushiriki kama wakufunzi, wakitumia uzoefu wao wa uongozi kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa kizazi kipya.

Mbali na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, mafunzo haya pia yanashirikisha Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, wawakilishi wa mashirika binafsi, pamoja na mabingwa wa masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka maeneo mbalimbali duniani.IMG-20250428-WA0228-1024x683 IMG-20250428-WA0230-1024x682 IMG-20250428-WA0227-1024x682 IMG-20250428-WA0231-1024x682 IMG-20250428-WA0229-1024x682

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *