Jeshi : NDC Watembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


22 Feb 2018

Jeshi : NDC Watembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza



Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Februari 21, 2018(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa akifanya mazungumzo mafupi na Maafisa Wakufunzi(hawapo pichani)kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Magereza leo Februari 21, 2018.

Maafisa Wakufunzi toka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza kabla ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kushoto) ni Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe.

Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitembelea sehemu mbalimbali katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.

Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa utambulisho mfupi kwa maafisa waandamizi wa Jeshi hilo mbele ya ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(NDC) wakimsikiliza Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(hayupo pichani).

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiangalia meza iliyotengenezwa katika Kiwanda cha Uselemala cha Gereza Kuu Ukonga katika ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.

Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(kulia) akipokea zawadi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza kutoka kwa Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(kushoto).

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Washiriki(waliosimama mstari wa nyuma) kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(wa pili kushoto walioketi) ni Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(wa pili toka kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga na wa kwanza kulia aliyeketi ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad