Profesa Innocent Ngalinda Mtaalam Mshauri wa takwimu akitoa mada katika warsha ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi iliyoandaliwa na Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ)ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini ili kutatua changamoto zinazokabili huduma ya Mama na mtoto, Warsha hiyo inafanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam
Bi. Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mada katika Warsha hiyo iliyojadili mambo mbalimbali yanayohusu kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na salama kwa mama na mtoto nchini.
Kutoka kushoto ni Tausi Sued kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International ya Marekani, Angelina Ballat kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International, Julieth MawallaKutoka Halmashauri ya Wilaya Ubungo na Sara Luaimay kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni wakifuatilia mjadala huo.
Anna Sawaki Ofisa Mawasiliano na Habari Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo katika warsha hiyo.
Dr Brenda Squetra D' Mello Daktari Mshauri wa Afya ya Mama na Mtoto Hospitali ya CCBRT akichangia mada katika warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo.
Bi. Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifuatilia mada pamoja na washiriki wengine katika warsha hiyo.
Bi. Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akitolea ufafanuzi kwa waandishi wa habari mambo mbalimbali yaliyojadiliwa katika warsha hiyo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KATIKA kuhakikisha Vifo vinavyotokana na uzazi kwa kina Mama vinapungua,Jamii imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina wataalamu ,kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo.
Hayo yamebainishwa na Mratibu Taifa wa Muungano wa UtepeMweupe na Uzazi Salama, Rose Mlay wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.
Amesema kuwa mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.
Mlay amesema kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24 vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo salama,
"Ripoti inaonyesha vifo vinaongezeka kutokana na kukosekana kwa vituo vya afya vyenye pamoja na wataamu kama nyumbani na kwenye vituo visivyo na watalaamu,unakuta sehemu hakuna vifaa vya kumsaidia Mama ili aweze kujifungua salama,na hii inasababisha vifo hivi kuongekezeka"
".Amesema jamii kama ingekuwa inampeleka Mzazi kwenye vituo vya afya vyenye ubora basi vifo hivi vingepungua ikiwezekana kumalizika kabisa"Amesema Mlay.
Mlay amesema Takwimu za hapo awali zilionyesha kuwa takribaniwanawake 8000 hufaliki kila mwaka kwa sababu ya Matatizo yanayotokana na Mimba na Uzazi lakini Takwimu hizo zimeongekeza hadi kufikia zaidia ya elfu 10 kwa mwaka .
Kwa upande wao Wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye Mkutano huo ,wameitaka serikali kuhakikisha inaongeza bajeti kwenye sekta ya Afya ambayo itavisaidia kwenye vituo vya Afya kuwepo kwa wakunga wenye welevu na ujuzi ambao watasaidia kupunguza vifo hivo.
No comments:
Post a Comment