Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt. Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.
Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.
Pia, Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia. Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika.
"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Ngamange alisema katika mtandao wanafanya miradi ya uhamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara.
Alisema waligundua Watanzania wengi wanalima lakini si kibishara ambapo wameanza na miradi mitano katika maeneo maalum kama Ruaha ambako waendesha kilimo cha Papai kwa kufuata taratibu zote za msingi za kilimo hai.
Aliongeza kuwa mradi huo utakaoanza na ekari 384 zitakazogawanywa katika mafungu ya ekari 32 na kupandwa katika utaratibu wa kili mwezi mara moja ili waweze kusambaza papai kwenye masoko makubwa.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui (katikati) amueleza jambo Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha (alienyosha mkono), Amani Matinya akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukumbwa shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.
Muonekano wa shamba hilo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakielekea kujionea maji yanayotoka Mto Lukosi unaotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiangalia mashine zinazovuta maji kutoka Mto Lukosi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Muonekano wa Mto Lukosi.
Mmoja wa wakulima wa eneo la Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa (kulia) akifafanua jinsi maji yanavyo sambazwa kwa wakulima.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakipanda kwenye basi tayari kuanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam. HABARI/ PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment