Afya : Naibu Spika, Dk. Tulia Awajulia Hali watoto Wanaosubiri kufanyiwa Upasuaji wa Moyo (JKCI) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Jun 2017

Afya : Naibu Spika, Dk. Tulia Awajulia Hali watoto Wanaosubiri kufanyiwa Upasuaji wa Moyo (JKCI)



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Doreen Sosthenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimtazama mtoto Johnson Raphael (6) akichora picha ya mtu wakati alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo ili kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Zuwena Said (4) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Abdukarim Mahilo (2) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo huku Mama wa mtoto Fatuma Bakari akiangalia.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea na Maria Gervas ambaye ni mama wa Doreen Sosthenes (3) anayelipiwa gharama za upasuaji wa Moyo na Tulia Trust Fund. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.



Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja akimuelezea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson magonjwa mbalimbali ya moyo yanayowasumbua watoto. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Dkt. Sulende Kubhoja.

Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI). Picha na Anna Nkinda wa JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad