Kilimo Kwanza : Benki ya Kilimo Yaombwa kutoa Mikopo Arusha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


13 May 2017

Kilimo Kwanza : Benki ya Kilimo Yaombwa kutoa Mikopo ArushaKatibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.


Na Mwandishi wetu,

Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili kuchagiza sekta ya kilimo mkoani humo.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.

Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.

Post Top Ad