Mfuko wa Jamii :LAPF yawalipa Bilioni 8.3 za fao la Uzazi wanachama wake waliojifungua - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.

Post Top Ad

14 Dec 2016

Mfuko wa Jamii :LAPF yawalipa Bilioni 8.3 za fao la Uzazi wanachama wake waliojifungua

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao la zazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.

Mfuko wa LAPF umeweza kulipa fao la uzazi kwa jumla ya wanchama elfu kumi Tangu mfuko huo uanze kulipa fao hilo kwa wanchama wake mwaka 2012.

Akiongea katika hafla hiyo Meneja wa LAPF, Kanda ya ziwa, Yessaya Mwakifulefule amesema LAPF imetumia zaidi ya shilingi bilioni 8.3 kulipa fao la uzazi kwa kina mama wanachama wa Mfuko huo.

Akikabidhi hundi ya malipo hayo kwa mwanachama Nchama Renatus ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Nansio Ukerewe,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ameupongeza mfuko wa LAPF kwa kuwajali wanachama wake na kulipa mafao kwa wakati.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akiwa amemapaka mtoto wa Mwanachama wa mfuko Nchama Renatus baada ya mama huyo na wenzake kukabidhiwa hundi zao za fao la uzazi. Jumla ya sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo mkoani Mwanza.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akiwa amemapaka mtoto wa Mwanachama wa mfuko Nchama Renatus (katikati) baada ya mama huyo na wenzake kukabidhiwa hundi zao za fao la uzazi. Jumla ya sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo mkoani Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akiwa amepakata mtoto wa mnufaika.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao la zazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.

Picha ya pamoja ya wanufaika na mgeni rasmi.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akisalimia.

Post Top Ad