Matukio : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ziarani China - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Dec 2016

Matukio : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ziarani China



Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE Bw. Li Yi akimueleza Balozi Seif nia ya Kampuni yake ya kutaka kuibadilisha Zanzibar kimajengo endapo itaendelea kupewa tenda za Ujenzi walipokutana Mjini Beijing China.

Balozi Seif akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE inayojenga Jumba la Treni Darajani Bw. Li Yi katika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Nchini China. Nyuma ya Bwana ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed.


Na Othman Khamis Ame, OMPR
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi inayoshughulikia miradi ya Ujenzi wa Bandari na Madaraja Makubwa ya China { CHEC} iko tayari wakati wowote kuanzia sasa kusubiri kuanza kwa harakati za ujenzi wa Bandari ya Mizigo ya Mpiga Duri Mjini Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bwana Li Yi akiambatana na Timu ya wahandisi wa Kampuni hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mjini Beijing Nchini China.
Bwana Li Yi alisema Wataalamu na wahandisi wa Kampuni yake wameshakamilisha taratibu zote za kufanya Utafiti wa ujenzi huo baada ya kupewa nafasi hiyo kufuatia tenda iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Mradi huo.
Alieleza kwamba Kampuni hiyo kongwe Duniani iliyoasisiwa mwaka 1837 hivi sasa imebadilika kiutendaji ndani ya kipindi cha miaka miwili kwa kuzingatia zaidi sheria na taratibu wa Kimataifa kitendo chacho kimeleta mafanikio makubwa kwa Kampuni kiasi cha kuweza kuaminiwa na Taasisi na Mataifa tofauti Duniani..
Bwana Li Yi alisema CHEC kwa sasa ina uwezo wa kuendesha miradi ya Uvuvi, huduma za Maji, majengo ya bishara kubwa { MALL }pamoja na miundombinu ya miradi ya umeme na hata kilimo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliufahamisha Uongozi wa Kampuni nhiyo ya CHEC kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina pingamizi yoyote kwa uwamuzi wao huo wa kujihusisha na miradi mengine ya kiuchumi.
Balozi Seif alisema chakuzingatia zaidi katika miradi yao mipya wanayotaka kuianzisha ni kuandika barua za maombi na kuziwasilisha kwa Mamlaka inayohusika na Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} kwa hatua zinazofaa.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake alifanya mazungumzo na Uongozi wa Kapuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya Mjini China chini ya Mwenyekiti wake wa Kanda ya Afrika Bwana Hu Bo.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Bwana Hu Bo alisema Kampuni ya CRJE imeamua kuibadilisha Zanzibar kimajengo mazuri yakiwa na hadhi ya kisasa inayokubalika Duniani endapo wataendelea kukabidhiwa tenda za kazi hizo.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyekiri uwezo mkubwa iliyonayo Kampuni hiyo ya Ujenzi ya CRJE baadaye mchana alionana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni Kubwa inayoongoza Duniani katika uendeshaji wa Miradi ya Umeme ya TBEA.
Balozi Seif aliueleza Uongozi huo wa TBEA chini ya Makamu wa Rais wake Bwana Wang Pinshan kwamba Wataalamu wa Taasisi hiyo wana fursa ya kuangalia namna wanavyoweza kuisaidia Zanzibar katika huduma mbadala ya nishati ya Umeme.

Post Top Ad