Habari : Mpiga Picha Maarufu Mpoki Bukuku Amefariki Dunia - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Dec 2016

Habari : Mpiga Picha Maarufu Mpoki Bukuku Amefariki Dunia


Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.

"Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo la Mwenge  ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas.

Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.

Post Top Ad