Mkurugenzi
wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw.
Mick Kiliba akiongoza mjadala katika kikao cha Mrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Mkurugenzi
Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya
Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kwa Wajumbe kutoka katika Wakala
mbalimbali za Serikali katika ukumbi wa Wakala za Serikali katika kikao
kilichofanyika ukumbi wa Wakala kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Katikati ni Mkurugenzi
wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw.
Mick Kiliba na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA), Bw. Dominic Rwekaza.
Baadhi ya washiriki kutoka Wakala Mbalimbali za Serikali wakifuatilia mada katika kikao chaMrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Kaimu Mtendaji
Mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo
akichangia mada kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya
Utendaji Kazi kwa Wakala mbalimbali za Serikali katika ukumbi wa Wakala
za Serikali katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Wakala kwa Njia ya
Mtandao (TaGLA) leo.
Serikali
imezitaka wakala zake kuwa na utaratibu wa kubadilishana uzoefu juu ya Mifumo
na Viwango ya Utendaji Kazi ili
kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Hayo
yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Idara
ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bwana Mick Kiliba
alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mrejesho wa
Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi vya Wakala za
Serikali kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala
ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Bwana
Kiliba alisema kuwa, Serikali imekuwa ikifanya maboresho katika nyanja
mbalimbali ikiwemo sekta ya Umma na kwamba moja ya mkakati wa kuboresha Utumishi
wa Umma ni pamoja na kuimarisha Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi.
“Mifumo na
Viwango vya Utendaji Kazi ndio msingi na nyenzo muhimu ya uwajibikaji na
uboreshaji wa utoaji wa huduma katika Taasisi za Umma zikiwemo Wakala za
Serikali,” Bwana Kiliba alisisitiza.
Alibainisha
kuwa, matumizi ya Mifumo na Viwango vya utendaji kazi katika Wakala za Serikali
ni jambo muhimu katika kufikia matarajio na malengo ya kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment