Na .Vero Ignatus ArushaWATUMISHI 71 walioomba ruhusa kwenda masomoni kutoka Halmashauri
za Arusha Vijijini na Meru mkoani Arusha, wamesababishia hasara ya
zaidi ya Sh milioni 837.5 baada ya kubainika hawapo masomoni.
Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Arumeru kwa kushirikiana na halmashauri hizo iliunda tume ndogo kujiridhisha kuwapo watumishi hao masomoni.
Iligundulika kuwa watumishi 306 waliomba kwenda masomoni katika vyuo vikuu mbalimbali nchini lakini kati yao, 71 hawapo vyuoni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Alexander Mnyeti, alisema watumishi hao wameendelea kupokea mishahara huku wengine wakilipiwa masomo yao na serikali bila kuwapo vyuoni.
“Tumebaini wengine waliaga kwenda masomoni kuanzia 2011 ila kutokana na kutokufuatiliwa hawajarudi mpaka sasa na wanaendelea kupokea mishahara.
“Wengine tunasikia wanafanya kazi katika NGO’S za watu binafsi, wakuu wa vyuo wametoa ushirikiano mkubwa kwa tume hiyo,” alisema Mnyeti.
Alisema katika Halmashauri ya Arusha Vijijini, hasara iliyosababishwa na watumishi hao ni zaidi ya Sh milioni 342 huku Halmashauri ya Meru ikipata hasara ya zaidi ya Sh milioni 495.
Aliwataka watumishi waliopo vyuoni ila wataona majina yao kwenye orodha hiyo, ndani ya siku 10 watoe taarifa na kuthibitishwa na wakuu wa vyuo wanavyotoka.
“Tunawapa siku 30 warudishe fedha hizo kwenye akaunti za waajiri wao ili fedha hizo zitumike katika shughuli nyingine za maendeleo.
“Walete risiti za malipo ya fedha hizo kabla serikali haijachukua hatua nyingine kwa sababu hawapo vyuoni wala kazini. Hivi watu wanaifanya serikali shamba la bibi?” alisema.
Alitaja vyuo hivyo ambavyo watumishi hao wamebainika hawapo kuwa ni Vyuo vikuu vya Arush,a Makumira, Mount Meru na Chuo cha Ualimu Patandi.
Vingine ni vyuo vikuu vya Ruaha Catholic, Teofilo Kisanji, SAUT Mbeya, Mzumbe, SUA, Jordan, SAUT Mwanza, Chuo cha Ualimu cha Eckernfodre Tanga, Sebstian Kolowa, Mwalimu Nyerere Memorial, Chuo kikuu Kampala International, Chuo cha Uhasibu.
Vingine ni vyuo vikuu vya Mwenge Catholic, Stephano Moshi na KCMC huku tume hiyo ikiwa bado haijenda katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
Mnyeti alisema baada ya watumishi hao kurejesha fedha hizo, hatua nyingine za sheria zitachukuliwa dhidi yao.