Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari
juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya
TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya
uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA
Sinza jijini Dar es Salaam. Mwasilishaji
mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa
waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za
usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA
Sinza jijini Dar es Salaam.Mmoja
wa watoa mada kutoka TAWLA akiwasilisha mada yake katika mafunzo ya
uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu
kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI Mtendaji
wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga
akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina kila
sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa
zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Alisema
licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine
kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa
kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia.
Alisema
wanawake wanaoachwa peke yao na familia wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa
wa familia jambo ambalo limeendelea kuwaingiza katika hali ngumu. Aidha
aliongeza kuwa pamoja na hayo ajali nyingi za waendesha pikipiki maarufu
kwa jina la bodaboda zimekuwa zikiwaathiri akina dada na akina mama
ambao ndio watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kiasi kikubwa.
Tamwa
katika mradi huo imejikita katika kutoa elimu ya madereva kuepuka
ulevi, ufungaji mikanda ya usalama katika magari, mwendo kasi na
matumizi ya kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao. Kwa
upande wake Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu
alisema suala la usalama barabarani si jukumu la taasisi moja hivyo
kila mtu anapaswa kushiriki katika kupambana na hatimaye kutokomeza
ajali hizo ambazo zimekuwa zikipoteza roho za watu, mali pamoja na
kusababisha ulemavu kwa baadhi ya waathirika wa ajali hizo.
No comments:
Post a Comment