Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) Dr.
JimYonazi wa Tatu kutoka Kushoto akifafanua jambo wakati Ujumbe wake
ulipofanya mazungumzo na Balozi Seif. ---------------------------------------------------------- |
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alivikumbusha vyombo
vya Habari Nchini kuanzisha utaratibu maalum wa kutumia sehemu ndogo ya
ukurasa wa Magazeti wanayochapisha kwa lugha za Kigeni ili kuwapa fursa
wageni pamoja na Watalii wanaohitaji kujifunza Lugha ya Kiswahili.
Alisema
lazima ufike wakati kwa Lugha ya Taifa Tanzania ya Kiswahili ienziwe
kwa nguvu zote chini ya usimamizi wa wataalamu wa lugha hiyo pamoja na
wana Habari kupitia vyombo wanavyofanyia kazi.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati akibadilishana mawazo na
Uongozi Mpya wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania {TSN }
ulioambatana na Uongozi wa Gazeti la Zanzibar Leo mazungumzo
yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema
kazi ya vyombo vya Habari wakati wote ni kuelimisha Jamii
inayovizunguuka vyombo hivyo. Hivyo lazima watendaji wake wanapaswa
kujitahidi kutumia kalamu zao katika kuupatia Habari, Taarifa pamoja na
Taaluma njema Umma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza watendaji wa Kampuni ya
Magazeti ya Serikali Tanzania {TSN }wanaochapisha magazeti ya Dailynews,
Sundaynews na Habari leo kwa kazi kubwa wayaoendelea kuitekeleza kwa
kipindi kirefu sasa Nchini Tanzania.
Alisema
Dailynews na Sundaynews ni mama wa magazeti Nchini Tanzania
yaliyofungua tasnia ya Magazeti ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki kwa
miaka mingi iliyopita.
Balozi
Seif alisema kwa kuzingatia ukongwe wa Magazeti hayo aliuomba Uongozi
Mpya wa Taasisi hiyo ya Habari Tanzania kuongeza Kuchapisha zaidi Habari
zinazolihusu Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili zieleweke upande wa
Tanzania Bara.
Akilizungumzia
Gazeti la Zanzibar Leo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema
Serikali inaangalia mbinu za fedha zitakazoliwezesha Gatei hilo kuwa na
mtambo wake wa kuchapisha Magazeti yao wenyewe.
Mapema
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania { TSN }
Dr. JimYonazi alimueleza Balozi Seif kwamba Kiswahili kinaweza kuuzwa
Kimataifa kwa vile hadi sasa hakuna Gazeti linalofundisha Lugha ya
Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dr.
Jim Yonazi alisema Lugha hiyo ambayo tayari inazungumzwa Kimataifa
katika maeneo mengi Duniani inaweza kutafsiriwa ndani ya magazeti katika
lugha nyengine za Kigeni kwa lengo la kutoa nafasi kwa Watu wanaotaka
kujifunza Lugha hiyo.
Mhariri
Mtendaji huyo wa Magazeti ya Serikali Tanzania aliitaka Jamii ibadilike
kufanya biashara ya kisasa kwa kutumia vyombo vya Habari kama magazeti
na hata Redio na TV kwa lengo la kukabiliana na mfumo wa Teknolojia ya
kisasa ya Habari na Mawasiliano.
Dr.
Jim alisema hivi sasa yapo mabadiliko makubwa ya mfumo wa Teknolojia ya
Mawasiliano kiasi kwamba wananchi wanastahiki kujifunza ili kuwepuka
kupita na wakati wa sasa unaokwenda kwa kasi Ulimwenguni.
Alieleza
kwamba Kapuni za Habari za Tanzania zinapaswa zikue zaidi kwa kusambaza
kazi zao nje ya Tanzania ili kupata fedha za kigeni zitakazosaidia
kumudu gharama za uzalishaji.
No comments:
Post a Comment