Uwajibikaji : Jamii Media Yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane " - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Aug 2016

Uwajibikaji : Jamii Media Yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane "


 Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane. Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau

Mkufunzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo 

akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.

Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura. 

Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.
Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.
Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.
Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.
Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.
Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.
Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.
Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.
Malengo ya Tushirikishane
Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:


i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.​


Matarajio ya Mradi
Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:


i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.​


 Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau
 Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.


 Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Mhe. Maxence Melo akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Bilele(CCM) na Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA).

Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.
 Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.
Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad