Matukio : WCF yawafikia Madaktari 380 ikijiandaa kuanza kutoa fidia julai mosi 2016 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Jun 2016

Matukio : WCF yawafikia Madaktari 380 ikijiandaa kuanza kutoa fidia julai mosi 2016



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba, akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, yanayofanyika mjini Mbeya Juni 13, 2016.Mafunzo hayo ni muendelezo wa kampeni ya WCF kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani, ILO, kuwapatia mafunzo Madaktari kote nchini, ili kujenga uwezowa kufanya tathmini ya madhara aliyoyapata mfanyakazimahala pa kazi kabla ya kupatiwa fidia. WCF itaanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi Kuanzia Julai 1, 2016. (PICHA ZOTE NA EMMANULE MADAFA)

 Baadhi ya madaktari waliohudhuria mafunzo hayo


KATIBU Tawala Wilaya ya Mbeya, Bi.Quip G. Mbeyela(pichani juu), amefungua mafunzo kwa madaktari kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya leo Juni 13, 2016 na kutoa rai kwa Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi kuhakikisha wanawashindanisha madaktari wote waliopewa mafunzo kuhusu ajali na magonjwa yanayotokana na kazi ili wale madaktari wataofanya vizuri waweze kupewa motisha.
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Shirika la Kazi Duniani, (ILO), imetoa mafunzo ka madaktari wapatao 380 kutoka katika hospitali za rufaa mikoani na wilayani Tanzania Bara. Zoezi hili limefanyika katika vituo vikumbwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na kumalizia na Jiji la Mbeya linalohusisha madaktari kutoka mikoa na halmashauri za Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Katavi.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uwekezaji ya Bodi Dkt. Francis Michael, ametoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha mpango thabiti wa kushughulikia masuala ya fidia pale wafanyakazi wanapoumia au kupata magonjwa kazini. Aidha, shukrani zangu pia ziufikie uongozi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli kwa kuwajali wafanyakazi wake, ambapo tayari kiasi cha asilimia 0.5% ya mshahara wa
kila Mfanyakazi wa Umma kimeshatengwa kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017
Nae Mkurugenzi Mkuu amesema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, utatoa Huduma na Mafao Bora ikiwemo huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha pamoja na malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki akiwa anatekeleza majukumu ya mwajiri wake.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) uko mbioni kuanza malipo ya fidia ifikapo tarehe 01 Julai 2016. Wanufaika na fidia itakayotolewa ni wafanyakazi wote Tanzania Bara walio katika sekta binafsi na sekta ya umma watakaoumia, kuugua ama kufariki kutoka na kazi.




 Picha ya pamoja ya uongozi wa mkoa wa Mbeya, viongozi wa WCF, Wataalamu wa ILO na madaktari
 Wataalamu wa ILO, (Kushoto) na Viongozi wa WCF
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uwekezaji ya Bodi Dkt. Francis Michael, akizungumza kwenye mafunzo hayo
 Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uwekezaji ya Bodi Dkt. Francis Michael, akizungumza kwenye mafunzo hayo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad