Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Mpoki Ulisubisya ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha
maslahi ya watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya
kiutendaji.Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani
inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa bidii.
“Nimefarijika
sana kuoana suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH
kwa kweli mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano
huu, lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na
maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
Akizungumza
kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa
hospitali hiyo imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi
kufikia Bilioni 4.
Pia
amesema katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa
kuongeza ICU ya watoto wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo
ya uzazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto .Kwa mujibu wa Profesa
Museru Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua
huduma za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
No comments:
Post a Comment