Vipindi
vya redio vya Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali
nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo
vinalenga kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya
kondomu na kuepukana na msongo rika.
Mfulilizo
huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan
wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio yao, changamoto
wanazopitia ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha
yao ya kila siku.
Mchezo
wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya
MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF.
Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na
wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi
zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa
vipindi vya Shuga.
Katika
kuboresha utoaji elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya
UNICEF pamoja na TACAIDS kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision
Production wanaendesha mafunzo elekezi kwa vituo vya radio za jamii,
mameneja wa radio shiriki, watangazaji na waandishi wa habari pamoja na
kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na Mkoa, ambapo warsha hii
inafanyika mkoani Iringa.
Radio
zitakazoshiriki katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni
Clouds FM, Nuru FM – Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja
na Furaha FM, Hope FM, Qibla Ten FM za Iringa.
Mratibu
wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS
Abubakari Magege akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga
katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza
kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.
Mwakilishi
wa UNICEF Alice Ijumba akijibu maswali ya washiriki wa kipindi cha
redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho
kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.
washiriki wa kipindi cha redio cha shuga wakifuatilia mada kutoka kwa
Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa
kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.
Waratibu
wa Shuga Radio drama series msimu wa pili - Pendo Laizer na David
Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya
wasikilizaji.
Mshiriki
akichangia mada katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho
kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.
Mratibu
wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa -
TACAIDS,Fadhila Mturi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya
ufunguzi wa semina elekezi.
No comments:
Post a Comment