Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisaini kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Nondo cha Kamal
Steels Ltd. kilichopo Chang'ombe, DSM, pembeni yake ni Gagan Gupta
ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji wa Kiwanda hicho.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akiangalia makopo yanayotumiwa na
Kiwanda cha Kamal kama nalighafi za kiwanda akiwa na uongozi wa kiwanda.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akimuangalia fundi wa kusawazisha chuma kwa kutumia Shaper Mashine.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akipanda Mti wa
kumbukumbu mara baada ya kukitembelea Kiwanda cha Kamal.
WAZIRI wa viwanda,biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango hapa nchini (TBS) kuhakikisha wale wote wanaotaka kuingiza vilainishi mitambo kutoka nje ya nchi wanatoa taarifa kabla ya tarehe 1 mwezi wa 5 mwaka huu ili kupambana na bidhaa bandia.
Mwijage ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika viwanda vitatu vya vilainishi mafuta na kiwanda kimoja cha nondo vilivyopo manispaa ya temeke jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa ziara hyo imelenga kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa bora na zinazokidhi mahitaji ya watumiaji wa bidhaa hizo.
Aidha Mwijage amewaagiza waendeshaji wa viwanda hivyo kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora kwani vilainishi mitambo vina umuhimu mkubwa sana hasa kudhibiti ajari mbalimbali katika mitambo ya uendeshaji shughuli za kimaendeleo.
Katika ziara hiyo mh. Mwijage alianza katika kiwanda cha nondo cha kamal steel, akaenda kiwanda cha vilainishi mitambo cha fuchs pia alienda katika kiwanda cha vilainishi mitambo cha general petroleum na kumalizia ziara yake katika kiwanda cha kuzalishilia vilainishi vya mitambo cha oryx vyote vikiwa manispaa ya temeke jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment