Matukio : Polisi wafyatua mabomu ya machozi mbele ya benki ya CRDB, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Mar 2016

Matukio : Polisi wafyatua mabomu ya machozi mbele ya benki ya CRDB, Jijini Dar




NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
POLISI wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu na wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlizni wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada ya mlizni kuona hivyo alitoa taarifa kituocha polisi Mbagala-Maturubai, nahapo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishanobaadaya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza kupigana nao.
Kuona hivyo wtu walianza kujaa na polisi bila kufanyaajizi wakafyatua mabomuya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki hiyo, palitokea tukio baya ya uvamizi wa benkiya Access ambapo watus aba waliauawa wakiwemo polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad