Mkurugenzi wa Mabibo Beer, James Lugemarila, (kulia), akziungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Bibi Josephine Simon Mshumbusi kwenye Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Machi 20, 2016. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi yatakayofanyika Jumanne Machi 22, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
MWILI
wa marehemu bibi Josephine K. Simon Mushumbusi umeagwa leoMachi 20, 2016 kwenye
kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Sala
na tayari umesafirishwa kwenda kijiji ni kwake, Kashura mkoani Kagera kwa
mazishi.
Mrehemu
Josephine ambaye alifariki Machi 18, 2016 baada ya kusumbuliwa na malaria kali
alizaliwa Mei 2, 1931 kwenye kijiji cha Kashura mkoani Kagera na ameacha watoto
kadhaa., .
Ibada
ya kuuaga mwili wa marehemu ilianza majira ya mchana na mamia ya wakazi wa
jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake walifika kwenye ibada hiyo, mtoto mkubwa
wa marehemu, ambaye ni Mfanyakazi wa UTT-PID, Euginia Simon, amesema mazishi ya
mama yake yatafanyika Jumanne Machi 22, 2016 kijijini alikozaliwa. Bwana alitoa
bwana alitwaa na jina lake lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment