Kutoka Kulia Phidesia Mwakitalima, katibu
wa Jumuiya ya wazazi ccm wilaya Arusha Rehema mohamed ,
Augustino
Masawe wawakilishi kamati ya utekelezaji wazazi wilaya ya Arusha wakiwa na
Afisa ustawi wa jamii jiji la Arusha Mussa mkamate katika
mazungumzo juu ya Mahabusu ya watoto
Arusha.
picha ikionyesha uchakavu wa vyoo vya mahabusu ya
watoto Arusha pamoja na pakti za viroba ambavyo wanakunywa
kisiri siri na kuletewa
kinyemela na vijana wa mtaani kutokana na kukosa ulinzi kwa
mahabusu hayo pia
kukosekana kwa uzio katika magereza hiyo ya watoto , na imeonekana pia
kuna matundu ya mapaa ya mabati ambayo ayapo pichani Matundu ambayo yamechakaa yanatumika na
watoto
hao kama njia ya kutorokea nje ambapo mara kadhaa
hukamatwa wakiwa wanatoroka na kurudishwa
ndani
Na Woinde
Shizza,Arusha
Kamati ya
utekelezaji Jumuia ya
wazazi wilaya ya Arusha inatarajia kutembelea
mahabusu ya watoto Arusha katika
kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi
Tanzania inayofanyika kila april 2 kila mwaka .
Katika
maazimisho hayo pia kamati
hiyo imejipanga kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya kituo cha mahabusu ya
watoto iliyopo jijini hapa .
Akizungumzia
maadhimisho hayo katibu
wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya
Arusha Rehema Mohamed alisema
wao kama wazazi wamegundua kuna changamoto
nyingi katika mahabusu ya watoto mkoani Arusha ambazo wazazi kama walezi
wameona ni vyema kutembelea mahabusu ya watoto kuwaona
na
kuwapelekea chochote kinachopatikana .
Alisema kuwa
wanajaribu pia kutatua changamoto nyingi
wanazokabiliana nazo
ili kuweza kuwasaidia watoto hao nao waishi kama watoto wengine walioko
majumbani .
“kwa kweli natoa wito kwa wazazi wote
watakaoguswa Arusha kujumuika nasi tar 2 mwezi wa nne kuanzia saa 3kamili
asubuhi kwani watoto wengine wazazi wao
wamewatelekeza kabisa na wengine hawana wazazi
kabisa”alisema Rehema
Kwa upande wake
mjumbe wa Kamati hiyo Phidesia
Mwakitalima alisema kuwa Watoto hawa wengine
wazazi wao hawaji kuwaona wengine hawana wazazi wanakabiliana na changamoto
nyingi sana ikiwemo pia kesi zao kwenda taratibu.
Mwakitalima
alisema kwa sababu watoto waliopo katika
mahabusu
hiyo ni watoto wenye haki ya
kupata elimu hivyo pia aliomba serekali ijaribu
kuwafikiria
watoto hawa ambao wapo mahabusu .
Ameongeza kuwa
endapo watoto hao
watapatiwa elimu wakiwemo mahabusu
itawasaida kwani hata wakiondoka hapo hawataondoka
bure na pia atatoka na elimu ambayo itamsaidia ata
akienda kuondoa ujinga mtaani na pia itamsaidia ata kutoweza kujiingiza katika
makundi mabaya ya mtaani kwani atakuwa na elimu kidogo ambayo itamsaida katika
maisha yake.
Aidha aliomba serekali pia iangalie
mahabusu
hiyo kwani watoto wengine kesi zao
zinasikilizwa mda mrefu bila suluhu na makosa mengine kisheria likifikishwa
mahakamani kesi inapaswa kuisha siku hiyo hiyo
“mfano hapa
kuna kesi ya mauaji
mtoto alimsaidia dada yake asichomwe kisu na shemeji yake akachukua kisu
akamuwahi shemeji yake na amekubali kosa lakini mwaka wa pili
mahakamani wanasema
ushahidi haujakamilika hivyo jamani naomba serekali iangalie sana hawa watoto
kwani mbali na yote wanateseka wasaidie angalau kesi zao zisikilizwe kwa wakati
na watendewe haki jamani kiukweli inauma naomba
serekali iwaangalie awa watoto jamani “alisema Phidesia
Aidha aliomba
serekali kuangalia kwa
makini sana mahabusu hii ya watoto kwani
mbali na hivi pia mahabusu hii watoto wakiumwa wanapelekwa hospital na pikipiki
hakuna gari ya mahabusu saa nyingine dawa zinakosekana na maafisa kujikuta
wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti usiwakute.
No comments:
Post a Comment