Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona akiwa anakata utepe ikiwa ni ishara ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo ya vito na madini
Wafanya
biashara wakubwa ambao ni wa pili kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya
Jacaranda Holding DR,Antony Haj Frisby akiwa na mwenzake wanachagua
madini ya vito kwa ajili ya kuyanunua ambapo alisema kuwa maonyesho haya
ni mazuri sana ila aliomba wachimbaji wadogo wajitokeze kwawingi
kuleta bidhaa zao.
Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona wa tatu kulia
akiwa anaonyeshwa moja ya madini ya vifo yalioletwa katika maonyesho ya
wafanyabiashara wa ndani wa madini hayo yaliyofanyika ndani ya mji mdogo
wa mirerani mkoani Manyara
Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer akiwa anaonyesha jiwe la Tanzanite ambalo lipo tayari kuuzwa.
Idha
benki ya NMB ilimefungua rasmi tawi katika mji huu ndogo wa mererani
hapa meneja wa mji mdogo wa benki hiyo akiwa anamueleza mkuu wa wialaya
pamoja na wananchi waliouthuria semina hiyo huduma ambazo wanazitoa
benki hiyo ndani ya mji mdogo wa mirerani
habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog,Mererani
Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza wote
waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la
usafirishaji bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa nguvu.
Inadaiwa kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za kuishi kwenye eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja kiubabe na kujiandaa kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa.
Akizungumza juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku
mbili yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa
kuwalipa fidia waliokuwa wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao waondoke.
Alisema baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa ujenzi utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za kuuza nje ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo.
Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo kwa mara ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana madini ya Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo hilo.
“Ni heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa
Mirerani, hivyo tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye
maonyesho haya ili kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona.
Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema
maonyesho kama hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya watu wana dhana potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani.
“Kupitia maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini
ya vito kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto nyingi zinazowakabili,” alisema Laizer.
Kwa upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias
Kayandabila alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo wa Mirerani na yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo.
Kayandabila alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa wa madini ya vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya kijani, Roadlite na mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao.
Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini kanda ya ya kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha madalali wa madini (Tasgedo) na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).
No comments:
Post a Comment