Meneja
wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi
Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo
cha Afya Misasi.Kulia ni Happness Manyenye, Ofisa Mwandamizi wa
PPFHafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.
Meneja
wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi
Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo
cha Afya Misasi.Hafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.Kushoto kwa
waziri ni Mkurugenzi wa Hlmahsuari ya Misungwi, Nathan Mshana.
PPF
Meneja.Meneja wa mfuko PPF,Meshach Bandawe kushotoka akizungunmza na
baadhi ya wananchi wa Misasi kabla ya kukabidhi msaada wa magodoro na
mashuka kwenye kituo cha Afya Misasi wa pili kutoka kujlia waliokaa ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ni Mbunge wa
jimbo la Misungwi,kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri wa Misungwi,
Nathan Mshana na wa pili ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,
Khalid Mbitiyaza.
Picha zote na Baltazar Mashaka.
Na Baltazar Mashaka,MWANZA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF umetatua moja ya changamoto za kituo cha Afya
Misasi,Wilayani Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutoa msaada wa magodoro
20 na mashuka 20,yenye thamani ya sh.3.5 .
Msaada
huo ulikabidhiwa jana kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga ambaye
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,hafka iliyofanyika katika kituo
hicho na kuhudhuriwa an Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi.
Akikabidhi
msaada huo, Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe,alisema mfuko
huo umekuwa ukisaidia jitihada za serikali kuboresha afya za jamii kwa
kutoa misaada mbalimbali katika sekta ay afya.
Alisema
wanafanya hivyo ili kuwasaidia na kuwawezesha wanachama wa mfuko huo
wawe na afya bora ili waweze kuchangia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na
kuwakinga na majanga wawapo kwenye ajira.
“Msaada
huu wa magodoro 20 na mashuka 20 licha ya kuwa si mkubwa utapunguza
changamoto za kituo hiki cha Afya Misasi,na ni sehemu ya kuisadia
serikali yetu kuboresha afya za wananchi wake na uwekezaji wa
mfuko,”alisema Bandawe
Alimwomba
Waziri na Mbunge huyo kuwa, awasaidie kutoa elimu kwa jamii ijunge na
mfuko huo ili wanufaike na mafao yanatolewa na PPF kwa kuwakinga na
majanga,ili pindi wakistaafua wasipate taabu baada ya kuwa wamekosa
nguvu ya kufanya uzalishaji.
“Walimu,Walikuma
na Wafugaji wanaweza kujiunga na mfuko kwa ujtaratibu maalum wa
kujichangia,hivyo tunakuomba Mbunge utusaidie kutoa elimu kwa wananchi
na kuwahamasisha wajiunge na mfuko wetu,”alisema Bandawe.
Naye
Kitwanga akipokea msaada huo,aliushukuru mfuko huo akisema umepunguza
kero ya magodoro na mashuka lakini pia marafiki zake wa nchini Australia
wamesaidia kituo hicho kinachohudumia wilaya tatu za Kwimba, Shinyanga
na Misungwi yenyewe, vitanda vya kisasa 16 vyenye thamani ya sh.16
milioni.
Alisema
vifaa vizito kulingana na mahitaji ya kituo hicho vinatokana na bajeti
ya wilaya kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha tiba bora kwa
wananchi zinapatikana kwa karibu.
“Tunahitaji
vituo vya Afya kila Kata,hata kituo cha Misasi kinachohudumia baadhi ya
vijiji vya wilaya za Shinyanga, Kwimba na Misungwi, kikipanuliwa bado
hakitakidhi mahitaji isipokua msongamano utapungua.”alisema
Alisema
Serikali itaendelea kuajiri Madaktari na Wauguzi kulingana na bajeti
ambapo kwa sasa kituo hicho kina madaktari 14 kutoka wawili wa awali
tangu kilipoanzishwa mwaka 1968.
Awali
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dk.Ernest Celestine alisema kuwa kituo
hicho kinakabiliwa na ukosefu wa majengo ya wodi wagonjwa wanawake na
wanaume wanaofanyiwa upasuaji,magodoro na vitanda,ongezeko la wagonjwa
wa huduma za upasuaji,wagonjwa wa nje na wa kulazwa, wagonjwa wa Kifua
Kikuu(TB) na Virusi vya Ukimwi (VVU) .
Alisema
wanakabiliwa pia na ukosefu wa wodi ya kulala watoto,mashine ya Utra
Sound,makazi duni ya watumishi,huduma endelevu za maabara,jengo na
jokofu la kuhifadhi maiti,jengo la kuchoma taka hatarishi,jengo la
utawala na jiko.
No comments:
Post a Comment