Health : Saratani ya Kizazi na Kirusi cha Papilloma - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Jan 2016

Health : Saratani ya Kizazi na Kirusi cha Papilloma

Dk. P Vijay Anand Reddy mshauri mwandamizi na mkurugenzi wa kliniki ya
upasuaji kutoka Hospitali ya Apollo, Hyderabad.

Na Mwandishi wetu,
Ikiwa mwezi huu wa Januari ni mwezi maalumu kwa ajili ya kuhamasisha
mapambano dhidi ya saratani ya kizazi, wanawake wanashauriwa kufanya
vipimo vya uchunguzi kujua afya zao na kuwa msaada kwa wengine pia.
Kwa mujibu wa Dk. P Vijay Anand Reddy kutoka Hospitali za Apollo;
saratani ya kizazi inatibika kirahisi kama ikigundulika mapema.

Saratani ya kizazi huanzia kwenye sehemu ya chini ya mji wa mimba
ambayo inaunganisha na uke. Hii inasababishwa na ukuaji usio sahihi wa
seli ambazo zina uwezo wa kusambaa sehemu nyingine za mwili. Kirusi
cha (HPV) papilloma kinachosambazwa kwa njia ya kujamiiana ndicho
kisababishi kikuu cha saratani hii ya kizazi. Licha maambukizi mengi
ya kirusi hiki hayaonyeshi dalili za ugonjwa, kuendelea kwa maambukizi
haya katika sehemu za siri za mwanamke ndio kunaleta zaidi saratani
hii ya kizazi kwa wanawake. Kimsingi kwa asilimia 99 maambukuzi yote
ya saratani hii yanahusisha kujamiiana na kupata virusi hivi vya
papilloma (HPV) ambavyo ni maarufu katika eneo hilo la uzazi.

Kila mwaka wanawake 530,000 ulimwenguni wanakutwa na saratani ya
kizazi, wastani wa 275,000 wanafariki kwa ugonjwa huo, na 88% ya vifo
vinatokea katika nchi zinazoendelea (kwa mujibu wa Globocan 2008
upande wa taarifa za saratani, Januari 2012). Tanzania ina kiasi
kikubwa cha namba ya waathirika wa saratani hii kwa upande wa Afrika
mashariki na hata kwa ulimwengu, kwa mujibu wa taarifa za afya za hivi
karibuni.

Mwaka 2009, saratani ya kizazi ilichukua asilimia 35.3 kwa saratani
zote za wagonjwa kutoka hospitali ya Ocean Road. Inakadiriwa kuwa
asilimia 80 ya wagonjwa wanaogundulika wana ugonjwa wa saratani ya
kizazi hufariki ndani ya miaka 5 baada ya ugunduzi.

Dk. P Vijay Anand Reddy mshauri mwandamizi na mkurugenzi wa kliniki ya
upasuaji kutoka Hospitali ya Apollo, Hyderabad anafafanua kwamba
“saratani ya kizazi ni sababu inayoongoza katika vifo
vinavyosababishwa na saratani katika nchi zinazoendelea. Matukio mengi
yameendelea kutokea kwenye mikusanyiko ya watu wasiofanya vipimo vya
saratani hii mara kwa mara pamoja na sehemu zenye asili ya maambukizi
ya virusi hawa na pia maeneo yenye mitazamo mibovu ya zamani kuhusu
masuala ya kujamiiana.

“Kirusi cha (HPV) papilloma kimeundwa kwa vinasaba viwili kwa mpigo,
hivyo kinasambaa kwa kasi kupitia kujamiiana na mtu aliyeathrika na
virusi hao. Maambukizi
haya kwa njia ya kujamiiana yanaangukia kwenye kundi la hatarishi ya
kiwango cha chini na hatarishi kwa kiwango cha juu. Hatarishi ya
kiwango cha chini kitaalam ni (6, 11) na haisababishi saratani, wakati
hatarishi ya kiwango cha juu ni (16, 18) ambazo zinasababisha
saratani. Inakadiriwa kuwa zaidi ya 90% ya saratani ya kizazi
inasababishwa na HPV na kwa sasa inachukuliwa ndio chanzo kikuu cha
saratani hii” Aliongeza Dk. P Vijay Anand Reddy.

Chanjo za kinga mbili zimeweza kugundulika. Ya kwanza inalenga HPV
aina ya 6, 11, 16 na 18. Na chanjo ya pili inadhibiti zaidi aina ya 16
na 18. Chanjo hizi zimejaribiwa na kuthibitishwa na mamlaka ya vyakula
na madawa (FDA) kutoka Marekani na pia wakala wa madawa kutoka Ulaya
(EMA). Furaha iliyopatikana kutokana na upatikanaji wa chanjo ni kubwa
ukilinganisha kuwa nusu ya wanawake milioni wanapata saratani hii ya
kizazi na nusu yao hufariki.

Bado kwa Tanzania kuna namna tofauti ya kuepuka saratani hii kwa
kufanya vipimo kama ilivyoshauriwa na shirika la afya duniani (WHO),
ugunduzi ukionesha saratani ipo katika hatua ya kwanza ni rahisi
kuitibu kwa asilimia 100. Vipimo vinafanyika kila baada ya miaka
mitatu na wanawake wote walio na umri zaidi ya miaka 25 wanatakiwa
wapate vipimo hivyo.

Hospitali ya Muhimbili mara nyingi hufanya vipimo hivi kwa kutumia
njia ya  pap-smear, ocean road wanafanya kwa kutumia njia ya VIA na
VILI, na hospitali za mikoani kama KCMC iliyopo kilimanjaro. Hakuna
maumivu katika kufanya vipimo hivi na inachukua dakika 10 hadi 15 tu
ambazo zinaweza kukuongezea zaidi ya miaka 25 ukilinganisha na wale
walioathirika na saratani hii ya kizazi.

Dk. P Vijay Anand Reddy kutoka hospitali za Apollo Hyderabad India
amehitimisha kwamba “kimsingi wanawake wanatakiwa kupata chanjo hiyo
kabla hawajabobea kwenye zoezi la kujamiiana na kupata virusi vya HPV.
Na wanawake hawa wanatakiwa kupata chanjo hii ila haitawasaidia sana
kama tayari wameshapata virusi vya HPV. Licha saratani ya kizazi
inaepukika na inatibika, bado wanawake wengi hawana taarifa sahihi za
huduma za afya na matibabu kutokana na kutokuwa na maarifa na uhaba wa
vituo vya afya kwa nchi nyingi hasa kwa kufanya vipimo vya saratani ya
kizazi”
Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma
za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji
isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo
hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa
wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo
katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga
kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya
Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa
magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya
wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na
matatizo ya uti wa mgongo.

Post Top Ad