WANAFUNZI
538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo
katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.
Wameaswa hayo na Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane
ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere.
amesema
kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu kwani
wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.
Chuo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha
mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani
chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa
chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafali ya nane ya
chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere
leo jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika
mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho
ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar
es Salaam leo.Wanafunzi
wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika
katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akiwatunukia vyeti wanafunzi
waliofanya vizuri katika masomo yao katika mahafali yaliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wahadhiri
wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafali ya
nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam.
kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo
Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.
Picha na Avila Kakingo.
No comments:
Post a Comment