Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Saz Salula, akizungumza kutoa shukurani
wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili
ya Mhe. Makamu wa Rais kuagana na Watumishi wa Ofisi yake. Hafla hiyo
ilifanyika juzi Okt 20, 2015 kwenye Makazi ya Dkt. Bilal
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Saz Salula,
wakati wa hafla fupi ya kuagana na watumishi wa ofisi yake, iliyofanyika
Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Watumishi wa Ofisi yake (baadhi hawapo pichani) wakati
wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam,
juzi Okt 20, 2015.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakimsikiliza Dkt.Bilal, wakati alipokuwa akizungumza kwenye Hafla hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake baada
ya hafla hiyo.
Picha na OMR
MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa ushirikiano waliompa katika
kipindi chote cha miaka mitano kiasi cha kuweza kutekeleza majukumu ya
msingi ya ofisi hiyo ya kudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira kwa
ufanisi mkubwa.
Akizungumuza
katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es salaam
Dkt. Bilal alisema kuwa, anayo furaha kufikia kipindi hiki na kwamba
alifanya majukumu yake vema kutokana na kuwa na wasaidizi mahiri na
waliojitoa kufanya kazi zao kwa weledi na uvumilivu mkubwa muda wote.
“Natumia
nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote. Walinisaidia sana katika
kipindi nikifanya kazi ya kuitumikia nchi yangu. Niwashukuru ninyi
wafanyakazi wa ofisi yangu, mlifanya kazi kwa kujituma sana na majukumu
yetu kwa mujibu wa taratibu tuliyatekeleza kwa ufanisi,” alisema
Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza:
“Nakutakieni
kila la kheri katika utendaji wenu. Jitahidini kufanya kama mlivyofanya
kwangu kwa yule atakayekuja baada yangu. Nakushukuruni kwa zawadi hasa
ya vitabu maana mimi ni muumini wa kusoma, nitavisoma”.
Dkt.
Bilal aliwaambia watumishi hao kuwa ushirikiano waliompa katika
utendaji wa kazi umewezesha kuzipatia ufumbuzi hoja mbali mbali za
muungano na kusema hoja zilizobaki zinafanyiwa kazi na zitapatiwa
ufumbuzi katika serikali ijayo.
Hoja
ambazo zipo katika hatua mbalimbali za kutafutiwa ufumbuzi ni pamoja na
Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na
Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na Faida ya Benki Kuu; Usajili wa vyombo
vya moto, Uchimbaji na Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asili na Mapendekezo
ya Tume ya Pamoja ya fedha.
Kwa
upande wa mazingira alisema katika kipindi chake Tanzania ilipata
nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Masuala ya Mazingira kwa viongozi wa Bara
la Afrika jambo ambalo limewezesha nchi kutoa mchango mkubwa katika
suala zima la uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika Bara la Afrika.
Hata
hivyo, Dkt. Bilal alionyesha wasiwasi wake katika eneo la usafi wa
mazingira na kuwataka watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana na taasisi
nyingine katika kuhakikisha usafi wa mazingira unapewa kipaumbele katika
maeneo yote nchini.
Mapema,
akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Bw. Sazi Salula alimshukuru Makamu wa Rais kwa uongozi wake ambao
umekuwa mwongozo kwa watumishi katika utendaji wao wa kazi na kumtakia
kila la heri katika kipindi cha kustaafu kwake.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment