Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Idd Ramadhan
Mapuri akiwasalimia wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo
pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar
es Saam.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay
akitoa neno la ufunguzi kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu
(hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo
jijini Dar es Saam.
Mkurugenzi
wa shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bw. Smart Daniel
akiwasilisha mada kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo
pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar
es Saam.
Baadhi
ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi
juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi
juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi
juu ya haki za wazee wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay wakati akitoa neno la
ufunguzi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa- Maelezo.
Na Eliphace Marwa - Maelezo
TUME
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania kwa kushirikiana Shirika
lisilo la kiserikali la Help Age Tanzania zinaujulisha umma kwamba
tarehe 21 Oktoba 2015 kutakuwa na maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu Afrika.
Maadhimisho
hayo yatakayofanyika katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam
ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na Mabalozi wa Afrika
watahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kulinda na kutetea haki za
wazee Tanzania.
Akizungumza
na Wazee na watetezi wa haki za binadamu, Katibu Mtendaji wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay amesema kuwa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora inawajibika Kitaifa kufuatilia hatua za
utekelezaji wa haki za binadamu hususani wazee ili waweze kuishi kwa
furaha, amani na usalama kinyume na sasa Ambapo wazee wamekuwa wakiuawa
kwa imani za kishirikina.
Maadhimisho
haya ya haki za Binadamu Afrika ni sehemu ya Mpango-Kazi wa Kitaifa wa
Haki za Binadamu ambao ni mkakati wa Serikali wa miaka mitano (2013 –
2017) wenye lengo la kutoa dira kwa Serikali yenyewe kwa maana ya
Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia na wananchi kwa
ujumla jinsi ya kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu ili
kuimarisha utawala bora nchini.
Naye
Mkurugenzi toka Shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bwana Smart
Daniel amesema kuwa kati ya nchi 96 Duniani Tanzania iko katika nafasi
ya 92 kwa kulinda haki za wazee kwa kuzingatia vigezo vya upatikanaji wa
huduma bora za afy, mazingira wezeshi kwa wazee, uhakika wa kipato kwa
wazee pamoja na uwezeshwaji wa wazee katika fursa mbalimbali ili
kujipatia kipato.
"Katika
suala la kipato Tanzania iko nafasi ya 94 kwa kujali wazee kwa kuwalipa
pensheni, katika suala la Afya kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 66 na
katika suala la mazingira wezeshi kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 88 na
hii inatokana na kutokuwepo kwa sheria ya wazee", alisema Bwana Smart.
Aidha,
Maadhimisho haya yanalenga kuongeza uelewa kwa umma juu ya wajibu
alionao kila mwananchi wa kutetea, kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha
haki za binadamu nchini ili kudumisha amani, utulivu na maendeleo
endelevu.
No comments:
Post a Comment