Mbali
na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio
kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.
Twende na Magufuli popote alipo.
Wananchi
wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za
Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka huu.
Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa kata ya Namalulu.
Vijana wa Kimaasai "Molan" wakiwa njiani kuelekea kwenye Mkutano wa Mwigulu Nchemba kata ya Loibosoit.
Mwigulu
Nchem akiwasili kata ya Loibosoit kwaajili ya kumuombea Kura Rais ajaye
wa awamu ya tano Ndg.J.Pombe Magufuli,Mbunge na Diwani wa Chama cha
Mapinduzi.
Wananchi wakiiitikia kuwa chaguo lao ni "kazi tu" wakimaanisha Magufuli kwa nafasi ya Urais.
Wananchi wakimsikiliza Miwgulu Nchemba.
wananchi wakichukua kumbukumbu za Mkutano wa hadhara wa Mwigulu NChemba wa kuinadi Ilani ya CCM.
Mwigulu Nchemba akiondoka kata ya Loibosoit.
Hatimaye Mwigulu Nchemba akawasili Jimbo la Kondoa Vijijini kata ya Kolo kuinadi ilani ya CCM.
Wananchi
wa kata ya Kolo wakishangiliwa ujumbe wa Mwigulu Nchemba kwao kuwa "CCM
imeamua kumleta Magufuli kwenye Nafasi ya Urais ili Mafisadi na
Walarushwa wakimuangalia waseme sasa rushwa basi,Lakini pia kwa wazembe
waanze kujiandaa kutafuta kazi ya kufanya kama hawatabadilika kwenye
serikali ya Magufuli"
Mwigulu Nchemba akimnadi Diwani wa kata ya Mondo jimbo la Chemba Ndg.Sambala.
Wananchi
wa Mondo wakimsikiliza Mwigulu Nchemba kwa makini,Kuwa mabadiliko
mazuri ya ya maendeleo sio vyama.Amewaomba wamchague Sambala aendelee na
ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Mondo,Lakini mradi wa maji mkubwa
umeshaanza kufanya kazi.
Mwigulu Nchemba akiondoka kata ya Mondo jioni ya leo.
Mwigulu Nchemba akishangiliwa mara baada ya kuwasili kata ya Kibaya Jimbo la kiteto.
Mwigulu
"Nawaonya wote wanaofanya siasa zisizo za kistaarabu,Vyama vya siasa
vipo kikatiba na Mikutano yake ipo kikatiba na Mavazi ya kila chama yapo
kikatiba,Nawaombeni kama mkutano sio wa chama chako ila unapenda kwenda
kusikiliza kinachozungumzwa jitahidi uwe mvumilivu,Ukianza kubishana na
wenye mkutano unajitafutia matatizo"
CCM
imemleta Magufuli kwa malengo,Kama Taifa tunataka kukomesha swala la
Rushwa,Kukomesha Utendaji wa kimazoea na Mbovu,Kukomesha Matapeli
wanaotoa mbole na pembejeo mbovu kwa wakulima na wafugaji,Mtu sahihi
anayeweza kushughulika na watu hao ni Magufuli tu.Nawaombeni mkamchague
Magufuli kwa Maendeleo ya kweli ya taifa letu".
Mamia
ya Wananchi wa Kiteto kata ya Kibaya wakimsikiliza Comrade Mwigulu
Nchemba jioni ya leo alipofika Kumnadi Mbunge mtarajiwa Ndg.Papian wa
Chama cha Mapinduzi.
Mkutano
wa Mwisho kwa leo,Mwigulu Nchemba anamalizika kata ya Matui Jimbo la
Kiteto.Anawasisitiza Wananchi kuunganisha nguvu zao kumpigia kura
Magufuli kwa Urais,Ubunge na Udiwani pia uende kwa CCM.Ilani
inayotekelezeka kwa Jimbo la Kiteto na Nchi nzima ni ya chama cha
Mapinduzi. Picha na Sanga Festo Jr.
Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa kata ya Namalulu.

No comments:
Post a Comment