Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman
S. Suleiman (kulia) akipewa maelezo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari
Pugu, Godwin Ogweyo kuhusu utengenezaji wa kadi ambazo hazichafui
mazingira alipotembelea maonesho ya shughuli zinazofanywa na wanafunzi
hao alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 46 ya wanafuzi wa kidato
cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kulia kwake ni
Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman
S. Suleiman (katikati) akiongozwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu,
Jovinus Mutabuzi kukagua bweni la wanafunzi la Ujamaa alilokuwa akilala
alipokuwa mwanafunzi hapo miaka ya 70 wakati alipohudhuria sherehe za
Mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es
Salaam juzi (Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu Mwandamizi wa Taaluma, Simon
Chumila.
Wahitimu
wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam
wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman wakati
akiwasili ukumbini kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi
hao, shuleni hapo juzi (Oktoba 22).
Sehemu
ya wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Sekondari Pugu wakifuatilia
matukio ya sherehe za Mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne
yaliyohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman, shuleni hapo, Dar es
Salaam juzi (Oktoba 22).
Wazazi
wa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es
Salaam wakiwa wamesimama kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman
alipokuwa akiwasili kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi
hao shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania, Mhandisi Suleiman S. Suleiman akivishwa skafu na mwanafunzi wa
Shule ya Sekondari Pugu kama heshima ya kuwa mgeni rasmi katika sherehe za
mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi
(Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
No comments:
Post a Comment