|
Eng.Philbert
Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa
baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya
maonyesho. |
|
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho. |
|
Wageni wakijionea namna mradi wa matofali ya gharama nafuu ulivyowanufaisha wenyeji wanaozunguka mgodi wa Buzwagi. |
|
Wageni
wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya KALTIRE ambayo
imekuwa ikihudumia mgodi wa Buzwagi kwa kuwauzia matairi kwa ajili ya
mitambo ya uchimbaji mgodini hapo. |
|
Wageni
pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi wa Buzwagi na wale wa serikalini
wakijionea matairi makubwa yanayotumika katika mgodi huo. |
|
Wageni wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la PANAF |
|
Sehemu ya familia za wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wakiwa wameketi baada ya kutembelea mabanda mbalimbali |
|
Kama vile hawaamini!!!! Ni kweli anacheza na nyoka hivyo? |
|
Kuhakikisha kumbukumbu hii haipotei kamera za simu zikafanya kazi yake |
|
Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani safi ya Ngoma waliyoitoa. |
|
Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani ya ngoma |
|
Michel
Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia
akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi |
|
Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa maonyesho |
|
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na mkuu wa
kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya maonyesho |
|
Azael
Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa
wageni walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha
Mafunzo. |
|
Ufugali
wa nyuki wa kisasa ni moja kati ya shughuli zinazofanywa na mgodi wa
Buzwagi kupitia idara ya Mahusiano ya Jamii kwa kuwawezesha wenyeji
wanaozunguka maeneo ya mgodi kujipatia shughuli zinazowaongezea kipato. |
|
Wataalamu
wa idara ya afya wakionyesha baadhi ya vifaa mbalimbali vinavyotumika
kupima afya za wafanyakazi wakati wote ili kuhakikisha afya za
wafanyakazi wa mgodi huo muda wote zinakuwa salama. |
|
Wataalamu
wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye dhahabu na namna
wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta dhahabu. |
|
Kikundi
cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma wakati wa
maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi |
|
Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi. |
Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati) na Meneja
wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa
zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi wa Mkuu
wa wilaya ya Kahama.
Meneja
Ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga akizungumza na
wafanyakazi wa Mgodi huo wakati alipokuwa akimkaribisha meneja Mkuu wa
mgodi wa Buzwagi.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza na
wafanyakazi wa Mgodi huo pamoja na familia zao wakati wa sherehe za siku
ya familia.
Watoto wakishiriki michezo mbalimbali iliyokuwepo maalum kwa ajili yao
Watoto wakishiriki michezo wakati wa sherehe hizo.
Graham
Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu (kushoto) akiteta jambo na
Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia
wakati wa sherehe hiyo
Mtaalamu wa masuala ya uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la idara yake.
Mmoja
wa wafanyakazi wa wa Idara ya masuala ya usalama wa Mgodi wa Buzwagi
akitoa maelezo kwa baadhi ya familia za watumishi wa mgodi huo wakati
walipo tembelea banda maalum la maonyesho la idara ya usalama mgodini.
Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi Bwana Moses Msofe akiwa na familia yake kusherekea siku ya familia
Wazazi wakiwasimamia watoto wao walipokuwa wakishiriki michezo mbalimbali ya watoto.
Watoto
wa baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi huo wakifurahia michezo mbalimbali
wakati walipokuwa wakiadhimisha siku ya familia mgodini hapo
Baadhi
ya ndugu wa wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakiangalia aina mbalimbali
za mashine zinazotumika katika shughuli za uchimbaji katika mgodi huo.
Moja kati ya magari makubwa kabisa yanayotumika katika mgodi huo likiwa katika eneo la maonyesho.
Kutoka
kushoto ni meneja wa uendelezaji wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanda,
katikati ni Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na Michelle
Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia wakati wa
sherehe za siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi.
|
Baadhi ya familia za watumishi wa Mgodi wa Buzwagi zikitambulishwa wakati wa hafla hiyo. |
Na Dixon Busagaga,Kahama.
Buzwagi
imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa
wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa
mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya
familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo
kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika
na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
Mwaka
huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea
shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na
mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo
ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe
hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji Michelle
Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa
masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na
mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa
serikali..
No comments:
Post a Comment