Mgeni
rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Septemba 26,1995, Jaji Mstaafu Osebia
Munuo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha
maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC
Kijitonyama Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC,
Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba.
Mgeni
rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jaji Mstaafu Osebia Munuo (kushoto),
akikata keki maalumu ya Maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika
Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa
LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba.
Wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya kuanza maadhimisho hayo.
Waimbaji wa Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya wakiimba wa wimbo wa Taifa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya ikifanya vitu vyake katika maadhimisho hayo.
Hapa
ni Kwaya ya Mwalusanya ikiserebuka kwa kwenda mbele. 'Jamaa wa mbele
kushoto yupo vizuri kiuchezaji chezea maadhimisho ya miaka 20 ya LHRC
wewe'
Mwenyekiti
wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari (katikati), akitoa hutuba fupi katika
maadhimisho hayo. Kulia ni Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi na kushoto ni Mgeni rasmi wa
hafla hiyo, Jaji Mstaafu, Osebia Munuo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba (katikati), akisoma hotuba yake
ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye.
Meza
Kuu ikionesha Kitabu cha Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa LHRC
baada ya kuzinduliwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mdau wa LHRC,
Profesa Chris Peter, Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye, Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC, Dk.Hellen Kijo-Bisimba, Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji
mstaafu, Osebia Munuo, Mwenyekiti wa Bodi LHRC, Geoffrey Mmari
na Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Rehema Ntimizi.
Mdau wa masuala ya haki za binadamu, Ally Said Mwashongo akichangia jambo kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi Jaji Osebia Munuo akisoma hotuba yake.
Wadau wakisoma kitabu hicho baada ya kuzinduliwa.
Wasanii wakicheza ngoma ya Mganda kwenye uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
MATUKIO
ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na vyombo vya dola
hususan jeshi la polisi hapa nchini yameongeza kufikia asilimia 60
imefahamika.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo -Bisimba Dar es Salaam jana katika
sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa LHRC Septemba
26, 1995.
"Matukio
ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa vyombo vya dola bado yapo juu
ingawa uelewa kwa wananchi kuhusu haki za binadamu ni mkubwa
ukilinganisha na miaka ya nyuma wakati tunaanzisha LHRC" alisema Dk.
Bisimba.
Alisema
baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na
jeshi la polisi ni pamoja na kuua raia na kesi zinapofikishwa mahakama
zinashindwa kuendelea kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi.
Dk.
Bisimba alisema matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na
wananchi hasa familia ni asilimia 40 ambapo wamekuwa wakijichukulia
sheria mkononi ya kuua watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali pamoja
na kuvamia vituo vya polisi na kupora silaha.
Alisema
katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa LHRC jamii imekuwa na
uelewa mkubwa wa matukio ya kifisadi yaliyowahi kutokea kama Sakata la
Epa, Richmond, ununuzi wa ndege ya rais, mfuko wa kufufua uchumi na
Escrow.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo Jaji Mstaafu Osebia Munuo alitoa pongezi kwa
LHRC kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kutetea haki za
binadamu.
Munuo
alikiomba kituo hicho na mashirika mengine kuendelea kuhamasisha
wananchi waliojiandikisha kujitokeza kwenda kupiga kura wakati utakapo
wadia na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu amani ya
nchi yetu.
"Naamini
sauti ya kituo cheni cha LHRC ni kubwa hivyo baso muitumie vizuri
kuhakikisha makundi yote katika jamii yanashiriki vyema katika uchaguzi
mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu bila ya kubaguliwa" alisema Jaji
Munuo.
No comments:
Post a Comment