Waziri
wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa
ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akimsikiliza Mhandisi
wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Ephraim Mushi wakati
alipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira
Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Wanafunzi
kutoka shule za msingi mbalimbali jijini Tanga, wakiangalia madini ya
ujenzi wakati walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano jijiji Tanga.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Mhe.
Stephen Masele, akiongea jambo wakati alipotembelea banda la Wizara ya
Nishati na Madini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Afisa
Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Innocent Makomba (kulia)
akiwaeleza akiwaonesha wananchi waliofika katika Banda la Wizara ya
Nishati na Madini madini ya ujenzi aina Uranga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Dunian yanayoendelea katika Viwanja vya Tangamano Jijijini Tanga.
Waziri
wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa
ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akisalimiana na
wananchi na watumishi wa sekta mbalimbali baada ya kuwasili katika
viwanja vya Tangamano jijini Tanga kufungua maonesho ya Siku ya
Mazingira .
Na Asteria Muhozya, Tanga.
Kampuni
za uchimbaji madini, utafutaji mafuta na gesi wakiwemo wachimbaji
wadogo nchini, wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi wa
mazingira wakati wanapotekeleza shughuli zao, ili kuwezesha rasilimali
zinazopatikana ardhini ziweze kuwa endelevu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Rai hiyo imetolewa na na
Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ephraim Mushi
wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yanayoendelea
kufanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini, Tanga.
Mhandisi
Mushi ameeleza kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu
duniani hususan katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ni muhimu mahitaji yao yakaenda sambamba na rasilimali zilizopo.
“Nafahamu
uelewa wa makampuni ya uchimbaji madini na utafutaji wa mafuta na gesi
katika usimamizi na kutunzaji wa mazingira ni mkubwa, kwani tayari kampuni
hizo zina mpango wa usimamizi mazingira ambao umeeleza masuala
yanayopaswa kuzingatiwa, lakini bado wanapaswa kuzingatia jambo hili
wakati wote kutokana na umuhimu wa wake”, alieleza Mushi.
Kuhusu
wachimbaji wadogo ameeleza kuwa, bado wanafanya shughuli zao za
uchimbaji bila kuzingatia sheria na kanuni za usimamizi wa mazingira.
“Wachimbaji wadogo bado hawazingatii suala hili lakini Wizara inafanya
jitihada mbalimbali za mara kwa mara kuhakikisha wachimbaji wanafuata
taratibu ikiwemo kuwaelimisha kuhusu usalama na mazingira”,aliongeza.
Hivyo, amewataka wachimbaji wadogo kuwa na mpango wa utunzaji mazigira kwa kuwa utaonesha namna ya kuhifadhi na kutunza mazingira na hivyo kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni husika.
Akieleza zaidi kuhusu jitihada zinazofanywa na wizara katika kusimamia masuala ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira, hususan katika sekta za nishati na madini, ameeleza
kuwa, Wizara imeshatoa mafunzo kadhaa kuhusu masuala hayo kwa maafisa
mazingira mazingira wa halmashauri katika Wilaya mbalimbali za mikoa ya Mwanza, Iringa na Mbeya kuhusu sheria na kanuni za madini na athari za uchimbaji usiozingatia uhifadhi mazingira.
Vilevile ameongeza kuwa, wizara
mafunzo mengine ni pamoja na mpango kazi wa mazingira wa wizara ambapo
maafisa mazingira hao wanatakiwa kuingiza masuala ya madini kwenye
mpango kazi yao. Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kuendelea kufanyika
katika miningine katika mwaka wa fedha ujao.
Aidha, ameeleza kuwa,
wizara imekuwa ikishirikiana na taasisi kadhaa zenye uhusiano wa
masuala mazingira kama vile Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) na wizara nyingine katika masuala yanayohusu miradi ya nishati na madini jambo ambalo limeleta matokeo mazuri kwa kuwa miradi yote ya nishati na madini haiwezi kuanza bila kufanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira.
Siku ya mazingira duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 1 - 5 Juni, ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu “ Ndoto Bilioni Saba. Dunia Moja. Tumia Rasilimali kwa Uangalifu”. Aidha, maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na tarehe 1 Mei,2015, na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb)kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal.
No comments:
Post a Comment