
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi
Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la
Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini
Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu
216 wa Mafunzo hayo.


Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la
Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza.

Kikundi
cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha
Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest
Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi
Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.

Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini matukio
mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la
Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji,
Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga,
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza).
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride Maalum
lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la
Pili ambayo yamefungwa rasmi Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu
wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya
Mgeni rasmi IGP Ernest Mangu(hayupo pichani) katika mwendo wa haraka
wakitoa heshima leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza
Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216 wamehitimu Mafunzo
Uongozi Daraja la Pili na kupandishwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya heshima
kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi
Daraja la Pili(kushoto katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja.

Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akifurahia
onesho Maalum la Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi Maalum cha
Kutuliza Ghasia Magerezani(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Ernest Mangu(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji,
Sylivester Ambokile wakifurahia onesho hilo kama wanavyoonekana katika
picha.
No comments:
Post a Comment