Matukio : Wafanyakazi Wahimizwa Kujitokeza Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 1 May 2015

demo-image

Matukio : Wafanyakazi Wahimizwa Kujitokeza Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


20150501034512
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.
Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
20150501034516
 Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
20150501034522
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
20150501034523
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais - Ikulu...
20150501034537
20150501034559
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania...
20150501034601
20150501034614
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km. Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa wa Zamani (Picha na Christina Njovu).

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *