Mwenyekiti
wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na
kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za
kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel
nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo
ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[l] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali. |
Dr.Pendo akifanya mahojiano machache na Mheshimiwa Emmanuel kuhusiana na Filamu za kitanzania ambazo zitakuwa ziliuzwa mitandaoni pipote duniani. |
Mwenyekiti wa Proin Promotion Tanzania ndugu Johson Lukaza [r] akiwa na viongozi wa Kitanzania nchi Ubelgiji katika sherehe za uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania onlione. |
Kiongozi wa watanzania nchini Ubelgiji bwana Macha[r] akiwa na kiongozi wa watanzania jijini Antwerpen kwenye uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online popote duniani |
Mwenyekiti wa Proin Promotion bwana Johnson Lukaza [l] akiwa na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online jijini Brussel nchini Ubelgiji hapo jana. |
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mheshimiwa Dr.Kamala akibadilishana mawazo na wageni wake mara tu baada ya uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online duniani kote.Balozi ni mmoja wa washiriki waliofanikisha shughuli nzima ya uzinduzi huo. |
Warembo kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kwenye uzinduzi huo hapo jana.kwa manunuzi ya filamu zote za kitanzania sasa waweza kununua popote pale duniani kwa kutembelea website hii ya www.proinpromotions.co.tz Pendelea vya kwenu kwa kununua vyenu,sheme Watanzania,Warundi,Wanyarwanda,Wakongo,Wazambia,Waganda,Wakenya na waafrika woote tunaomba ushirikiano wenu kwa kununua filamu zetu sasa. |
No comments:
Post a Comment