Mdau
wa maendeleo, Jackson Kiswaga (mwenye skafu) akiwakabidhi moja ya
mabati 50 wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda kwa ajili
ya ukarabati wa jengo la taaluma na nidhamu lilounguamwaka 2013 katika shule hiyo.(picha na Denis Mlowe)
Mkurugenzi
wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akikabidhi cheti kwa
mhitimu wa shule ya shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda kidato cha
sita.
Mkurugenzi
wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akikagua gwaride wa skauti
wa shule ya shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda
Mkurugenzi
wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akizungumza wanafunzi na
wazazi wa shule ya shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda
Mkurugenzi
wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akivishwa skafu na moja ya
skauti wa shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda
NA DENIS MLOWE, IFUNDA
WAZAZI
wa wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda iliyoko
wilaya ya Iringa wamechangia mifuko ya saruji na misumari kwa ajili ya
kuunga mkono ukarabati wa jengo la taaluma na nidhamu liloungua katika
shule hiyo mchango wenye thamani ya shilingi 600,000.
Michango
hiyo ambayo ilijumuisha fedha taslimu kwa lengo la kununua saruji na
misumari ilitokana na juhudi za mgeni rasmi Jackson Kiswaga wa mahafari
ya 14 ya shule hiyo ya kidato cha sita kuhamasisha ujenzi wa jengo hilo
baada ya taarifa kutoka kwa mkuu wa shule Madi Kissuu aliyotoa kwa
wazazi na kukabiliwa na changamoto ya ujenzi baada ya kuungua kwa moto.
Akizungumza
katika mahafari hayo, Kiswaga ambaye alichangia mabati 50 papo hapo ili
zisaidie katika ukarabati wa jengo hilo lililoungua moto mwaka 2013
alisema kuwa jukumu la uchangiaji wa sekta ya elimu sio kuachiwa
serikali bali la kila mzazi anayependa maendeleo ya elimu katika nchi ya
Tanzania.
Alisema
wanafunzi ni lazima wasome kwa bidii ili watengeneze maisha yao ya
baadaye kwani elimu ndio urithi pekee usiofananishwa na mali zingine za
dunia kwani ni wa kudumu katika maisha yote ya binadamu hivyo juhudi ya
mzazi kumuunga mkono mtoto katika kupata elimu iliyo bora na katika
mazingira rafiki kwa mwanafunzi.
Kiswaga
aliwataka wanafunzi hao kuacha tabia hatarishi zikiwemo utoro, uzinzi,
ulevi na kila aina ya mambo yanayorudisha nyuma uelewa wao katika masomo
shuleni hapo.
“Hakuna
mtu mjinga dunia kama sio kichaa au una tatizo la ubongo. Kumbukeni
kuwa MUNGU aliweka masaa 24 na kila mmoja akitumia saa 24 kwa uhakika
katika maisha yake lazima kuna mambo ambayo atafanya kuweza kujiletea
maendeleo yake na wanafunzi pia mna masaa hayo hayo ni wakati wako sasa
kuamua unataka kuwa nani kesho na njia pekee ni kushikilia masomo na
hapo ndipo ukichagua yaliyo mazuri unaweza kubadilisha maisha yako na ya
jamii inayomzunguka,” alisema.
Alisema
Tanzania inahitaji wasomi ili ijiletee maendeleo na kushindana kiuchumi
na nchi nyingine hivyo ni muhimu wanafunzi wakaendelea kuhimili vikwazo
wakati wakitafuta elimu zao.
Kwa
upande wake Mchungaji Kedi Patrick kutoka nchini Uganda aliyeambatana na
mgeni rasmi Jackson Kiswaga, aliwataka wazazi na wanafunzi kutambua
kuwa elimu ndio chanzo kikubwa cha mabadiliko katika taifa lolote hapa
duniani.
Alisema
kuwa urithi pekee kwa watoto ni elimu na kusisitiza kuwa unaweza
kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo
urithi pekee.
Naye
mkuu wa shule hiyo, Madi Kissu alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changomoto nyingi zinazohitaji juhudi za pamoja kuzitatua hasa katika
uchakavu wa majengo na kukosekanika kwa walimu wa masomo ya sayansi.
Katika
mahafari hayo ya 14 jumla ya wanafunzi 324 wanatarajia kumaliza elimu
ya kidato cha sita yaliambatana na gwaride la heshima lilotolewa na
skauti wa shule hiyo sambamba na kukabidhiwa vyeti kwa wanafunzi wote na
zawadi kwa walimu waliofanya vizuri katika kufaulisha masomo yao.
No comments:
Post a Comment