Teknolojia : Tigo Yazindua Huduma ya Intaneti ya Kasi Zaidi 4G LTE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 25 April 2015

Teknolojia : Tigo Yazindua Huduma ya Intaneti ya Kasi Zaidi 4G LTE


Muonekano katika duka la Tigo mlimani city ambapo wateja walishuhudia jinsi gani mtandao huu wa kasi wa intaneti unavyofanya kazi kwa kuona matukio laivu kwa kutumia mtandao wa intaneti Kampuni ya simu Tigo Tanzania leo imezindua teknolojia mpya ijulikanayo kama 4G LTE ambayo utaifanya kuwa  mtandao wa intaneti wenye kasi zaidi kuliko yote nchini Tanzania 
wafanyakazi wa tigo ,wageni waaalikwa na wasanii maarufu wa Bongo fleva wakifuatilia matukio yanayoendelea katika uzinduzi wa teknolojia hii ya kasi zaidi ya mtandao wa intaneti ya 4G lte toka kampuni ya tigo


Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii na baadhi ya wafanyakazi wa  Tigo wakiwa katika picha ya Pamoja 

Msanii wa bongo fleva Fid q  akijadili jambo na MC wa hafla hii ya kuzindua intaneti ya kasi kwa teknolojia ya 4g lte 
washereheshaji wa hafla hii ya kuzindua intaneti ya kasi zaidi nchini toka tigo hapa mliman city 
wafanyakazi toka kampuni ya huawei wakipozi katika uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi nchini kwa teknolojia mpya ya 4G lte toka Tigo pekee
Baadhi ya wafanyakazi wa tigo na wageni waaalikwa wakishuhudia uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi nchini kwa kutumia teknolojia mpya ya 4G LTE toka tigo pekee



Mkuu wa uendeshaji na biashara  wa samsung Suleiman mohamed akieleza jambo kwa wafanyakazi jinsi gani wana vifaa vizuri vitakavyoendana na teknolojia mpya ya 4G lte toka tigo



burudani zikiendelea katika uzinduzi huu wa intaneti wa kasi zaidi wa 4G LTE  toka tigo pekee

Mkurungezi mkuu wa TCRA Prof John Nkoma akitoa hotuba pia Alitoa pongezi kwa kampuni ya tigo kwa kufanikisha mawasiliano ya intaneti kwa kasi zaidi pia kuendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi pia aliwasihi watanzania kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa maendeleo zaidi na kuboresha biashara zao

Waziri wa teknolojia na mawasiliano Mh Prof Makame Mbarawa akitoa hotuba katika hafla ya kuzindua intaneti ya kasi zaidi hapa nchini kwa teknolojia ya 4G lte toka Tigo pekee leo Mlimani city

Msanii wa bongo fleva Richmavoko akitumbuiza huku video yake ikioneshwa laivu kupitia youtube kwa muonekano bora zaidi ( HD ) kutokana na mtandao wa kasi zaidi wa intaneti wa 4G LTE Toka TIgo  Tanzania pekeee

Mkuu wa vifaa na intaneti wa Tigo David Zakaria akieeleza jinsi gani wateja wa intaneti watafurahia matumizi ya intaneti na jinsi walivyojiandaa kuwafikia watanzania wengi zaidi katika mkoa wa dar es salaam na mikoa zaidi ya sita kabla ya mwaka huu kuisha 

wageni waalikwa wakishuhudia jinsi gani mtandao huu wa intaneti ya kasi toka tigo unavyofanya kazi 

Msanii wa bongo fleva vanesa mdee akipata taswiraz "SELFIE" na mmoja wa wafanyakazi wa samsung katika uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi Tanzania leo Mliman city jijini Dar es salaam

Mmoja wa watu waliohudhuria hafla hii ya kuzindua mtandao wa kasi zaidi wa intaneti toka tigo wa 4g lte akipata maelekezo toka kwa mfanyakazi wa tigo jinsi anavyoweza kuijunga na huduma hiyo


Waziri wa teknolojia na mawasiliano mh ,prof Makame Mbarawa akifanya mahojiano na vyombo vya habari baada kuzindua teknolojia ya kasi katika mtandao wa intaneti 4G LTE pembeni ni mkurungezi mkuu wa TCRA Prof John Nkoma
   
Picha zote na   Krantz Mwantepele na Mathias Manyanya   wa Mwanaharakati Mzalendo Media        

No comments:

Post a Comment