Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu
wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah
Othman Ali wakati wa hafla ya kuyafunga mafunzo hayo hapo Skuli ya
Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kati kati yao ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis,
na nyuma ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi unaoondesha mafunzo hayo
Nd.Abdi Hamid Abeid.
Mkuu
wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah
Othman Ali akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea Darasa la
mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge.
Baadhi
ya Wanafuzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar
wakishuhudiwa na Balozi Seif wakiendelea kufanya mazoezi ya vitendo
katika kukabiliana na matatizo madogo madogo yanayojichomoza wakati wa
matumizi wa kompyuta zao.
Mmoja
wa Wanafunzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar
akiperuzi kuangalia nini kimejiri duniani kupitia mtandao wa Internet
akishuhudiwa na Balozi Seif.
Baadhi
ya Wananchi na Wanafunzi wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi Balozi
Seif hayupo pichani wakati akiyafunga mafunzo ya miezi mitatu ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar hapo Skuli ya Sekondari
Donge.
Balozi
Seif akimkabidhi Cheti Mwenyekiti wa Jumuiya Kupambana na changamoto
na kuwaendeleza Vijana Zanzibar Bibi Umukulthum kwa kusaidia uendeshaji
wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano.
Kati kati yao ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar
Maalim Khamis Mussa, na kushoto ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi wa
Mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mkuu
wa Mafunzo hayo Nd. Abdulla Othman Ali.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Donge, walimu
na wanafunzi wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano
yaliyokuwa yakifanyika katika skuli ya Sekondari ya Donge.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge ambae pia ni
Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamuhuna, Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya ZAFAYCO Bibi Umukulthum.
Kulia ya Balozi Seif ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis,
Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd.
Abdullah Othman Ali pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo
Zanzibar Maalim Khamis Mussa.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Vijana
wanaojifunza Taaluma ya Mitandao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
kuwa makini katika matumizi bora ya mfumo huo mpya ili kulinda mila na
Tamaduni zao za asili.
Alisema
si vyema kuthubutu kufanya matumizi maovu way mfumo huo akijua kwamba
yatawashawishi kujiingiza katika matendo yatakayowapelekea kuwa na
maamuzi ya kufanya vitendo vilivyo nje ya utamaduni wao.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akiyafunga Mafunzo ya Miezi
Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar { TEKNOHAMA }
yaliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar {
UMUZA } na Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana
Zanzibar { ZAFAYCO } hapo katika Majengo ya Skuli ya
Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema
Dunia imekuwa na Mabadiliko makubwa ya Teknolojia ya Kisasa ya
Mawasiliano inayokwenda kwa haraka kiasi kwamba Jamii za Kimataifa
popote pale zilipo hupata fursa za kuwasiliana, kushirikiana na hata
kupashana taarifa kupitia mfumo huo.
Akisoma
Risala Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nd.
Abdullah Othman Ali alisema kwa kuelewa matatizo na changamoto
zinazowakabili vijana katika maeneo mbali mbali Nchini Taasisi hizo
zimebuni mradi huo kwa kuwakusanya pamoja vijana ili kuwapatia mafunzo
yanayowawezesha kujiepuisha na makundi maovu.
Naye
Mratibu wa Mradi wa mafunzo hayo wa Jumuiya ya kupambana na changamoto
na kuwaendeleza Vijana Zanzibar { ZAFAYCO } Nd. Abdi Hamid Abeid
alisema Jamii inaweza kupunguza uchafuzi wa mazingira endapo itakijika
katika katumizi zaidi ya Kompyuta.
Alisema
Wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Vyuo Vikuu hivi sasa wamekuwa
wakitumia kumbu kumbu za vitabu na baadhi ya maandisi na machapisho
kupitia mtandao huo badala ya mfumo wa zamani wa kutumia vitabu
vilivyokuwa vikitengenezwa kwa karatasi zinazotokana na kukatwa kwa
miti.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment