|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Urusi
nchini Tanzania, Mhe. Yuri Fedorovich Popov. |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb). akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Urusi mara baada ya
kupokea Nakala za Hati za Utambulisho. Katika mazungumzo hayo pamoja na
mambo mengine, Mhe. Waziri aliishukuru Serikali ya Urusi kwa misaada
inayotoa kwa Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile elimu. Wawili
hao pia waliafikiana umuhimu wa kukuza na kuimarisha zaidi ushirikiano
kati ya Tanzania na Urusi. |
|
Mazungumzo yanaendelea. |
|
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania. |
|
Waziri
Membe katikati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa
Urusi. Wakwanza kulia ni Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya
Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na kutoka kushoto ni maafisa wa Ubalozi wa Urusi nchini
Tanzania. |
============================================
BALOZI MTEULE WA ALGERIA
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Algeria
nchini Tanzania, Mhe.Saad Belabed. |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Membe alieleza kuwa zaidi ya miaka 50 sasa
Tanzania na Algeria zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano mzuri wa
nchi na nchi na hata katika ngazi ya Kimataifa kama vile Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika. |
|
Mazungumzo yakiendelea |
|
Mazungumzo
yanaendelea huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa kwanza kushoto), Bi. Zuhura
Bundala na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi
Kasiga wakinukuu mazungumzo hayo. |
|
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.Picha na Reginald Philip. |
No comments:
Post a Comment