Matukio : Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Wahamasisha Amani Kabla ya Uchaguzi Mkuu, Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 13 April 2015

Matukio : Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Wahamasisha Amani Kabla ya Uchaguzi Mkuu, Arusha

SAM_1708
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha, Daudi Ntibenda,akifungua mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_1679 
Onesmo Ole Ngulumwa, Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu akizungumza katika mkutano huo wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha, Daudi Ntibenda, kushoto Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala ya amani nchini Marekani, Steve Hege 
SAM_1695 Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala ya amani nchini Marekani, Steve Hege akizungumza katika mkutano huo.
SAM_1686
Wadau kutoka Taasisi za kiraia 
SAM_1681
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole kulia akifatilia mkutano huo
SAM_1709
Amani Golugwa mwenyekiti  wa CHADEMA mkoa wa Arusha akifatilia mkutano kwa umakini wakati mgeni rasmi akizungumza katika  mkutano huo
SAM_1685
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada SAM_1683
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada
SAM_1715
Picha ya pamoja
SAM_1719
Wadau wakipiga picha ya pamojana mgeni rasmi.

Waandishi wa habari hapa Nchini wametakiwa kuwaelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani katika nchi ya Tanzania tunapoelekea uchaguzi mkuu kwa kuandika na kutangaza amani hali itakayosaidia uchaguzi kufanyika kwa amani

Akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu,uliofanyika jijini Arusha mwisho mwa wiki, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa Arusha Husna Mwilima alisema kuwa uvunjifu wa amani una madhara makubwa sana katika nchi

Alisema kuwa vyombo vya habari vinajukumu kubwa la kuelimisha umma madhara ya vita hasa tunapoelekea uchanguzi mkuuu wa Rais,wabunge na madiwani,huku akitaka Tanzania kuiga mfano wa Kenya ambapo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikuwa vikitangaza na kuandika amani kipindi cha uchaguzi

Mwilima amewaomba viongozi wa vyama vya siasa, dini na taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana kueleza wafuasi wao juu ya umuhimu wa kutunza amani wakati wa uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu Onesmo Ole Ngulumwa alisema kuwa marekebisho ya baadhi ya mambo kabla ya uchaguzi mkuu ni muhimu ili kufanyika uchaguzi salama na yenye kujali demokrasia 
Pia aliongeza kuwa kwa kuwepo kwa amani itasaidia sana wananchi kupiga kura katika hali ya kiusalama zaidi

No comments:

Post a Comment