Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili
ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC,
uliofunguliwa Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,
Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa
dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa Aprili
29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe,
kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (AU), Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akitoa hotuba yake,
wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama
wa SDC, uliofunguliwa Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa
Viwanda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifuatilia hotuba ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akifungua
rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC,
uliofunguliwa Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
Baadhi
ya Mawaziri wa Tanzania, waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa
makini Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akisoma hotuba ya
ufunguzi rasmi wa Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa
SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Jumatano Aprili 29, 2015, ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa
dharura wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini
Harare, chini ya Uenyekiti wa Rais Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe,
Mwenyekiti wa sasa wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Mkutano
huo wa siku moja pia umehudhuriwa na Rais Seretse Ian Khama, Rais wa
Botswana na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mfalme Muswati III wa Swaziland,
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Namibia Hage Geingob, Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Watu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Rais wa Afrika Kusini
Jacob Zuma na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Awali
akifungua mkutano huo Rais Mugabe alisisitiza umuhimu wa nchi za SADC
kuwa na mpango madhubuti wa Viwanda kwa kuwa uwepo wa viwanda utasaidia
kupunguza tatizo kubwa linalozikabili nchi hizi hasa ajira, pamoja na
uchumi duni unaotokana na ukosefu wa viwanda vya kuboresha bidhaa
zinazozalishwa katika nchi za ukanda huu.
Mkakati
huu uliopitishwa na Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) unaanza mwaka huu 2015 hadi mwaka 2063. Katika mkakati huu
nchi za SADC zinalenga kutanua uhuru wa soko katika utatu wa kanda za
Kibiashara yaani SADC, EAC na COMESA ikiwa ni pamoja na kutenga eneo
huru la ukanda wa kiuchumi wa nchi za kanda hizi, huku lengo likiwa
kufanikiwa upatikanaji wa eneo huru la ukanda wa biashara kwa nchi za
Afrika. Masuala mengine ni pamoja na kukuza bidhaa zinazozalishwa katika
nchi hizi katika masoko ya Asia ambao ni walaji na watumaji wakubwa wa
malighafi zinazozalishwa katika nchi hizi.
Rais
Mugabe alifafanua pia kuwa, nchi hizi kwa umoja wake zikiunganishwa
utakuta ndizo zina rasimali kubwa ya madini ya Dhahabu, Almasi na hata
Gesi na kwamba kama mtengamano huu utakamilika nguvu ya pamoja inaweza
kugeuza hali ya maisha ya wananchi wa nchi hizi sambamba na maendeleo ya
kiuchumi katika nchi hizo.
Awali
akizungumza kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Mugabe, Katibu Mtendaji
wa SADC Dkt. Stargomena Lawrence Tax aliishukuru serikali ya Zimbabwe
kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu ambao ulikuwa ni mwendelezo wa ule
uliofanyika Victoria Falls, Zimbabwe Agosti 17, 2014 mkutano uliotaka
nchi wanachama wa SADC pamoja na kupitisha mkakati wake wa Kimaendeleo,
upange dira ya utanuaji na uendedlezaji viwanda katika ukanda huu.
Matukio
mengine katika mkutano huu ni pamoja na makabidhiano ya Kituo cha
Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, makabidhiano yaliyofanywa
na nchi ya Zimbabwe chini ya Rais wake Robert Mugabe kwa Katibu
Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo
hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha
vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani
ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia
migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Pia
Rais Mugabe alitumia muda huo kuutaka Mkutano huu wa Dharura kutoa
heshima zao kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyewahi
kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi kwa kutambua mchango wake katika
uhuru wa nchi zilizomo SADC na pia mchango wake kwa ajili ya maendeleo
ya nchi hizi.
Raia
Mugabe alimtaja Hayati Brigedia Mbita kama mpiganaji mahiri na kiongozi
aliyefanya kazi kwa maslahi ya watu wengi bila kuchoka na kwamba Afrika
na SADC vitamkumbuka daima kwa mchango wake huo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Harare, Zimbabwe
Aprili 29, 2015
No comments:
Post a Comment