Mjasiriamali na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja wa wajasiliamali ambaye pia ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake wa jinsi alivyo nufaika na mafunzo kama haya na mpaka sasa anajitegemea na Kupata kipatochake na kuwasaidia wengine.
Wa kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada ambaye amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi wake umuhimu wa mikutano kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata elimu Bora ya Kilimo.
Bwana Daniel Ambaye ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake katika maswala ya kilimo.
Mwendeshaji msaidizi wa Semina Hiyo Bwana Saidi akitoa mafunzo ya juu ya kuanzisha kilimo kwa kutumia Green House pamoja na faida zake
Bize akichukua yale ya Muhimu kabisa katika semina hiyo.
Wanasemina wakiwa wanasikiliza kwa makina mada mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa
Semina ikiwa inaendelea
Baadhi ya wanasemina wakiwa katika Picha ya pamoja
Kilimo na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary David Kinong'o.
Katika Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.
Pia walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi, Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.
Mwisho Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.
Tembelea Libeneke lake la: www.kukuprojecttz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment